beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,881
- 6,377
Polisi Mkoani Kusini Pemba inamshikilia Daktari mstaafu Nassor Khalid kwa tuhuma za kujaribu kumtoa mimba ya miezi mitatu Sabina Othman (21) Mkazi wa Tibirinzi Kisiwani Pemba
Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Hassan Nassir amesema tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Mgagadu na Daktari huyo hutumia nyumba aliyorithi kwa Babu yake kuwatoa Wasichana mimba
Amesema baada ya kupata taarifa waliweka mtego na kumnasa akiwa na Sabina ndani pamoja na Makame Vuai (aliyempa mimba Sabina) na walikuta pia sindano na dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kuzuia maumivu