Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
Na Jabir Idrissa
WAHAFIDHINA wa Zanzibar wamechomwa miiba mioyoni. Hawataki kusikia madhambi ambayo kufanikiwa kwake kuna maslahi makubwa nao.
Hawataki mjadala wa matatizo yanayokabili uandikishaji wapiga kura. Labda wanajua ukitendwa kwa haki wameumia. Wanaogopa chama chao Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaanguka. Wanajua kinaangushika.
Tulikuwa kwenye ukumbi wa Mlingotini, katika Hoteli ya Mazsons, ndani ya Mji Mkongwe. Waliotukutanisha ni Kituo cha Demokrasia Tanzania Tanzania Centre for Democracy (TCD) ili kujadili matatizo hayo.
Mada iliyoandaliwa, "Demokrasia, Uandikishaji wa Wapiga kura na Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi" nimeipenda. Ni nzuri iliyokuja kwa wakati muafaka.
Uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) la Zanzibar kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010 wa kuchagua rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani Zanzibar, umekumbwa na masahibu.
Umekabiliwa na shutuma na lawama. Maelfu ya wananchi wanalalamika kunyimwa haki ya kuandikishwa. Maana yake watakosa kupiga kura.
Wanalalamikia kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi. Kwamba ndiyo tatizo la wao kukosa haki yao. Wengi wao wamenyimwa licha ya jitihada zao za kukiomba kwa wanaohusika. Hakuna anayewajali bali wanalaumiwa ni wakorofi.
Sheria ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 1985 inashurutisha mtu kuwa na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi ndipo aandikishwe kupiga kura.
Kitambulisho hiki kinachomaliza muda wa kutumika Agosti mwakani, kinatolewa kibaguzi; wengi wanaostahili kupewa, hawapewi. Bali wapo wasiostahili wanafuatwa nyumbani kulazimishwa wasajiliwe ili wakipate.
Wazanzibari wanaokataliwa kitambulisho wanaishia kudhalilishwa na kujeruhiwa kwa mabomu ya machozi yanayorushwa na askari polisi. Wakirudi makwao, wanakuta nyumba zao zimechomwa moto, mazao yao shambani yameteketezwa. Wanafunguliwa mashitaka mahakamani.
Tatizo sugu la Zanzibar wakati wa uchaguzi ni wananchi wengi kuwa katika upande wa kukosa. Watahangaika kwa nguvu nyingi na kupoteza muda mwingi kutafuta haki yao, lakini wanaishia kudhalilishwa.
Wakati Mkurugenzi wa Idara inayotoa vitambulisho, Mohamed Juma Ame anaendelea kusema ametoa vitambulisho kwa watu 503,895; maelfu ya wananchi wanakusanyika vituoni na kwenye ofisi za idara hiyo kuomba vitambulisho.
Sasa kuna ushauri wa wadau kwamba mkurugenzi aende majimboni na orodha ya aliowapa vitambulisho, aite kimoja kimoja na kuangalia nani atajitokeza.
Wadau wanasema kwa yule atakayebainika amepata kitambulisho na bado anadai kingine wakati hakuna taarifa kituo cha polisi kuwa amepoteza kitambulisho alichopewa awali, ashitakiwe mahakamani.
Lakini kwa vile vitambulisho atakavyobaki navyo, basi watafutwe wenyewe kupitia taarifa za uongo walizotoa ili nao washitakiwe kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha kitambulisho. Kutoa taarifa za uongo ili mtu apate kitambulisho ni kosa la jinai.
Angalau mkurugenzi amesema jambo moja zuri. Kwamba ofisi yake na hasa ofisi zilizoko wilayani, hazina uwezo wa kusajili watu kwa mkumbo. Vizuri.
Kinachotakiwa siyo kuwapuuza watu wanaotaka kitambulisho, bali ni kuwaandalia utaratibu mwanana ili wasajiliwe na kupewa kitambulisho maana, ni haki yao kwa mujibu wa sheria. Kama kweli serikali ina nia njema, ihakikishe hakuna anayekosa kuandikishwa kupiga kura.
Kwa jumla, uandikishaji wapiga kura unachechemea tangu ulipoanza 6 Agosti majimbo la Mkoa wa Kaskazini Pemba. Baada ya watu kuona hawaandikishwi kwa kukosa kitambulisho, wamehamasishana.
Wamegoma. Wanafika vituoni kuzuia wachache wenye vitambulisho nao wasiandikishwe. Wanatuhumu kuwa baadhi yao wamo wanachama wa CCM ambao walipewa vitambulisho bila kikwazo chochote. Wapo pia wachache hawana sifa za kupatiwa kitambulisho, wamepewa. Wenyeji wanasema "Haiwezekani waje kuingizwa katika daftari."
Katika jimbo la Tumbatu, Mkoa wa Kaskazini Unguja, wananchi bila ya kujali vyama vyao, na wamegawika katika CCM na CUF tu, wamegoma hawaendi kuandikisha, ingawa wana sababu nyingine wakiilaumu serikali kwa kuwapuuza kwa muda mrefu.
Haya ni mambo ambayo wahafidhina hawataki kuyasikia yanajadiliwa hadharani. Basi wakawa wamejipanga kuvuruga kongamano la TCD. Mwenyezi Mungu alililinda na lilimalizika salama.
Hafidh Ali Tahir, mbunge wa Dimani, alianza. Kabla ya mjadala kuanza, aliomba kutoa taarifa. Alikubaliwa. Akasema haelewi TCD ina mamlaka gani ya kujadili masuala ya uandikishaji wapiga kura.
Isitoshe, maazimio baada ya mjadala yatapelekwa wapi kwenye mamlaka ya kuyatafuatilia. Akaiponda mada, muwasilishaji wake na TCD wenyewe kwamba wamepotoka kwani majadiliano hayatakuwa na maana yoyote maana walioshutumiwa hawapo kujitetea.
Akadai waitwe na kuruhusiwa kutoa mada yao, ndipo mjadala ufanyike. Hafidh, mwanasoka na mwamuzi wa kimataifa mstaafu, alimrukia muwasilishaji mada, Salim Said Salim, mwandishi wa habari mwandamizi nchini akiwa amefanyia kazi vyombo vya kimataifa, eti ameegemea upande mmoja wa kulaumu serikali.
Akapata wenzake. Akaja Ussi Yahya Haji, mbunge wa zamani wa Chaani. Sasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM. Akaunga mkono hoja hiyo na kumpa Salim majina.
Wakaibuka wengine kama walishakubaliana kugomea mjadala na kujitahidi kuuvuruga si hivyo watoke. Akaja Ali Suleiman Ali (Shihata), mwakilishi aliyetoka Mikunguni na kuingia jimbo la Kwahani, ambalo katika uchaguzi uliopita, lilikuwa na kufuru katika uvurugaji kwani kura zilizopigwa zilipita idadi ya walioandikishwa.
Akapinga mada na mtoa mada. Akadai viongozi wa CUF wanavunja sheria kwa kuhamasisha wananchi wasiende kujiandikisha. Alisema hilo lazima lisemwe hadharani.
Akaja Yussuf Mohamed Yussuf, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, na mbunge wa zamani wa Mwembemakumbi. Akatoa ya kwake ya kuunga mkono hoja ya Hafidh. Alimbomoa Salim akimuita ni mtu wa upinzani.
Akaja Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz akamkosoa mtoa mada; Ali Mzee Ali, Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi na Mjumbe wa NEC hakubaki nyuma akasema kupinga mjadala kuanza.
Akaja kijana wa CCM, Matogo Juma Matogo, akapinga naye na kuhimiza sheria zifuatwe katika kila jambo. Hao ni wanasiasa. Uvumilivu ulimshinda hata ofisa mwandamizi katika serikali, Mohamed Juma Ame. Akalalamika mada imepotosha ukweli wa mambo kuhusu vitambulisho. Akahofia mjadala wa mada utakuwa ni kupoteza muda.
SOURCE: MWANAHALISI.