Zanzibar has new driving licence and number plates


UDUMU BABA! Ndio maana hatutaki shirikisho la Afrika Mashariki tunaogopa na sisi tutafanyiwa haya tunayowafanyia wenzetu kwa kisingizio cha umoja.
 
Na ndio maana wana haki ya kutoza kodi

Jamani hata manispaa zetu zina haki ya kutoza kodi sioni kama hivi ni vigezo vya zanzibar kuwa nchi, tusirudi nyuma kuanza kutafuta ili nchi iitwe nchi inahitaji vitu gani, tulishalimaliza hili. Dar es salaam City Council si wantoza kodi au hamjui? au kuna definition tofauti ya kodi ya zanzibar na kodi nyinginezo
 

Pamoja na tofauti ya sheria zinazosimamia magari kati ya Zanzibar na bara, bado Zanzibar haikubanwa haswa na utekelezaji wa sheria hii, na si kweli kuwa kupata kibali ni vigumu. Mtu anayeimport ZNZ kisheria anawajibika kuomba foreign permit, lakini watu wetu wala hawafanyi hivyo, wanapeta tu, na TRA inaona upuuzi kuwafuatilia hadi pale tu wanapotaka kubadili namba.

Umuhimu wa kulipia kodi ya ziada unatoka na ukweli kuwa, kwa mujibu wa TRA, Zanzibar hawalipi kodi fulani fulani za Muungano, lakini inabidi zilipwe kama gari linakuja kutumika bara.

Au la magari yenye namba za ZNZ yasingekuwepo bara. Mengi yaliachiwa kuingia kiholela na kuna wakati hata yakawa yanafanya biashara yakiwa na namba hizo kinyume cha sheria...Mamlaka kama TRA zinauona ugumu uliopo katika kutekeleza sheria hizi za magari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…