Zanzibar has new driving licence and number plates

Zanzibar has new driving licence and number plates

Sio kama magari ya kutoka Zanzibar yanachukuliwa kama ya kigeni, yanachukuliwa kama ndio kwanza yamekuwa imported. Hata ukiomba kibali cha muda hakipatikani. Hata hivyo, gari zinazotoka Kenya na nchi za jirani yanapatiwa vibali vya kutembea barabarani bila ya matatizo yoyte yale, udumu muungano....

UDUMU BABA! Ndio maana hatutaki shirikisho la Afrika Mashariki tunaogopa na sisi tutafanyiwa haya tunayowafanyia wenzetu kwa kisingizio cha umoja.
 
Na ndio maana wana haki ya kutoza kodi

Jamani hata manispaa zetu zina haki ya kutoza kodi sioni kama hivi ni vigezo vya zanzibar kuwa nchi, tusirudi nyuma kuanza kutafuta ili nchi iitwe nchi inahitaji vitu gani, tulishalimaliza hili. Dar es salaam City Council si wantoza kodi au hamjui? au kuna definition tofauti ya kodi ya zanzibar na kodi nyinginezo
 
Sio kama magari ya kutoka Zanzibar yanachukuliwa kama ya kigeni, yanachukuliwa kama ndio kwanza yamekuwa imported. Hata ukiomba kibali cha muda hakipatikani. Hata hivyo, gari zinazotoka Kenya na nchi za jirani yanapatiwa vibali vya kutembea barabarani bila ya matatizo yoyte yale, udumu muungano....

Pamoja na tofauti ya sheria zinazosimamia magari kati ya Zanzibar na bara, bado Zanzibar haikubanwa haswa na utekelezaji wa sheria hii, na si kweli kuwa kupata kibali ni vigumu. Mtu anayeimport ZNZ kisheria anawajibika kuomba foreign permit, lakini watu wetu wala hawafanyi hivyo, wanapeta tu, na TRA inaona upuuzi kuwafuatilia hadi pale tu wanapotaka kubadili namba.

Umuhimu wa kulipia kodi ya ziada unatoka na ukweli kuwa, kwa mujibu wa TRA, Zanzibar hawalipi kodi fulani fulani za Muungano, lakini inabidi zilipwe kama gari linakuja kutumika bara.

Au la magari yenye namba za ZNZ yasingekuwepo bara. Mengi yaliachiwa kuingia kiholela na kuna wakati hata yakawa yanafanya biashara yakiwa na namba hizo kinyume cha sheria...Mamlaka kama TRA zinauona ugumu uliopo katika kutekeleza sheria hizi za magari.
 
Back
Top Bottom