Zanzibar heroes yawa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya CECAFA baada kutoka suluhu na Kenya

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Zanzibar heroes imekuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya michuano ya Cecafa baada ya kutoka suluhu na Kenya kwenye uwanja wa Kenyatta, Machakos nchini Kenya.

Kufuatia mtanange wa leo kulazimisha sare hiyo tasa na Kenya, Zanzibar imefikisha pointi 7 huku wenyeji Kenya wakiwa na pointi 5.

Hongera sana Zanzibar, lau kama mkipata uanachama wa CAF kwa mara nyingine na FIFA yamkini Zanzibar heroes watakwenda World Cup na Afcon kabla ya Tanzania Bara.
 
Hongera sana ZNZ nawatakia ushindi mnono na mwisho mubebe cup. But Wakina sisi sio watu wa mpira,,,twendelee na politics
 
Aisee !! Mbona zanzibar kuna vipaji vingi sna vya mpira wa miguu kwanini wasitupie macho zaid na kuwapa support ili tufkie mbali kimichezo
Tusiwaone ni wala urojo tu jamani kiukwel ukienda zanzibar na kutembelea viwanja vya mpira wa miguu utaelewa kwamba kuna special talents lakin zinaishia kufia maskan tu kwa kukosa support
 
Mkuu nakuunga mkono nimewangalia zanzibar wako vizuri sana ,Tz bara sijui tuna shida gani!
 
Mkuu nakuunga mkono nimewangalia zanzibar wako vizuri sana ,Tz bara sijui tuna shida gani!
Niwahi kukaa zanzibar kwa kipind flani yaan unakuta watoto wana vipaji hatar hadi unashangaa kmaa huyu hakuna ma agent ambao wanaweza kumpeleka katk football academy zenye hadhi ya kitaifa au kimataifa yaan watoto wanacheza soccer safi lile lakiakil kabisa lakufunzwa, full ball control

Na pia huku main land unaweza kuta vipaji vipo ila vichache na vingi vinaharibiwa na football style ya vijana wa mtaan

Yaan wanacheza zaid pira la nguvu na sio akili ,yaani ukinusurika kuvunjika mkuu basi hauwez kuonekana hata na kuku
 

Naunga mkono hoja
 
Taifa stars lazima ijitoe fifa na caf kwa sababu suala la michezo sio la muungano, tanganyika stars ipo ,sasa kwa nini wanatunyima fursa yetu ya kikatiba
 
Kama sio fitna za muungano wazanzibari wangekuwa kwengine kwa kila kitu na ndio maana kila upande unapowakuta wako vyema na tatizo lao linakuwa ni siasa za tz na viongozi wao sio issues za kiufundi na uwezo, kuna siku nafkir tz itafika kuona haya kwa inayoifanyia hawa jamaa
 
Mimi ni mzazibar na vipaji vipo Vingi sana vya mpira kikubwa kinachorudisha nikuwa hawana support vijana wenyewe lkn wanacheza boli kinoma jamaa. Fikeni mjionee wenyewe.
 

Chukulia mfano tu misaada kutoka nje kama wanapewa znz, na kama wanapewa basi ni fungu dogo sana ukilinganisha na bara. Mimi kama m-bara lakini..Inshort wazanzibar hawatendewi haki for anything...ndio mana hili linchi linapata mitihani/misukosuko mingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…