Lakini jamani mbona Mashoga wanaoana toka miaka?.. Namkumbuka sana Shoga mmoja Alex (Ally) aliolewa miaka ya 80 na mzungu huko Ulaya, wakirudi Bongo wakipeta mjini bila taabu...
Mimi nadhani pamoja na mila na dini zetu lakini haya maswala yapo sana tu na hatuwezi kuyazuia isipokuwa kkama yatatumika kwa bendera za imani hizo. Nikiwa na maana Muislaam akitaka kufunga ndoa kiislaam basi hairuhusiwi, Mkristu vile vile, akiwa mwanao mzee una haki ya kukaa ndoa hiyo na kumkana mwanao iwe kumpa radhi au kumfukuza lakini huwezi kuzuia jambo hili kwa sababu halina sheria ktk serikali yetu..sijui kama nakosea lakini ndio mtazamo wangu.
Mbali na yote haya, Mashoga na wasagaji hesabu yao leo hii ni kubwa kupindukia.. Uharamu wa dini au mila ni vitu vilivyokwisha pitwa na wakati kwa mtazamo wao. Kwa hiyo sisi tunaopinga haya tuyakane ktk jumuiya zetu za dini na mila lakini inapofikia swala la Utaifa wakuu zangu sidhani kama tunawafunza kitu hawa jamaa zetu...
Nitarudia tena msemo wangu wa awali, Mimi kama Muislaam siwezi kumzuia Mkritu kula nguruwe hata kidogo pamoja na kwamba ni haramu kwangu, wala sintakataa urafiki, ujirani, undugu na kadhali ati kwa sababu anakula nguruwe. Na wala sidhani kama ni makosa zaidi kwa Muislaam kula nguruwe kwani Uharamu hauna dini ya kuzaliwa isipokuwa ni matendo yako ndiyo yanakufanya uwe Muislaam..
Hivyo basi, kwa imani yanmgu iwe ya dini au Mila zangu nitakataa katakata kula nguruwe, nitakataa nguruwe kupikwa nyumbani kwangu lakini siwezi kabisa kumzuia mtu mwingine asile nguruwe naweza tu Kumkanya na kumwambia athari zake.. Uchaguzi ni wake..
Ukiweza kutafsiri undani wa hili toka nguruwe kwenda Kisanvu cha kopo basi bila shaka utakuwa umenipata vizuri!