Zanzibar imepata wapi pesa ya ruzuku ya mafuta?

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
16,784
Reaction score
23,312
Wakati wa mchakato wa rasimu iliibuka hoja ya serikali tatu, Dr. Shein akiwa rais wa Zanzibar wakati huo alikuwa miongoni mwa watu walipinga Kwa madai mapato ya Zanzibar ni kidogo hivyo isingemudu gharama za uendeshaji serikali ya muungano.

Leo taarifa ya habari imetangaza hatua ya serikali ya Zanzibar kutoa ruzuku kwenye mafuta na kupeleka mafuta na diesel kuuzwa chini ya shilingi 3000.

Ni jambo la kupongeza lakini linaacha maswali kwanini Zanzibar wanadai hawana pesa ya kugharamikia serikali ya muungano ila Wana pesa ya kutoa ruzuku kwenye mafuta, pia kwanini bara imeshindikana au Kwa sababu tunabeba gharama za muungano.
 
Wenzenu wana wajomba zao Uarabuni,nyie Tanganyika wajomba zenu wako wapi!!
 
Kama halmashauri tu ya wilaya inaweza kutenga bajeti kuhudumia raia, unahoji Zanzibar kutoa ruzuku ya mafuta kwa Watanzania Zanzibar?

Hivi SMZ mnaichukuliaje? Kuhusu Muungano, dola ya Tanzania ilikwishaundwa 1964. Tuache maneno madogo madogo.🙏🙏🙏
 
Wakati wa mchakato wa rasimu iliibuka hoja ya serikali tatu, Dr. Shein akiwa rais wa Zanzibar wakati huo alikuwa miongoni mwa watu walipinga Kwa madai mapato ya Zanzibar ni kidogo hivyo isingemudu gharama za uendeshaji serikali ya muungano.

Leo taarifa ya habari imetangaza hatua ya serikali ya Zanzibar kutoa ruzuku kwenye mafuta na kupeleka mafuta na diesel kuuzwa chini ya shilingi 3000.

Ni jambo la kupongeza lakini linaacha maswali kwanini Zanzibar wanadai hawana pesa ya kugharamikia serikali ya muungano ila Wana pesa ya kutoa ruzuku kwenye mafuta, pia kwanini bara imeshindikana au Kwa sababu tunabeba gharama za muungano.
Ruzuku si lazima itoke mfukoni, hata kusamehe sehemu ya Kodi iliyatakiwa ilipwe ni ruzuku pia
 
Nyie yalipokuwa 3000/Lita wala hapakuwepo hata wazo la ruzuku.😁.

Halafu Rais anaibuka kuzungumzia picha za misafara yake kati ya mada zote za mitandaoni!
 
Back
Top Bottom