Zanzibar inachangia nini kwenye Serikali ya Muungano? Isije ikawa wanatumia Kodi za Bara

Watanganyika nyie Hamna serikali,kuna serikali ya muungano na serikali ya Zanzibar..yaani ni kama li-nchi lenu mmelitelekeza,haya ndo matokeo...
 
Unajuaje Wabara ndio wanautaka zaidi?

Ni lini wananchi wa Bara a waliulizwa wakasema wanautaka huu Muungano ?


Na ni lini Wazanzibar walisema hawautaki?
Unajua sababu ya Uamsho kuwa ndani? Ndio utapata jibu kuwa wazanzibari wanautaka au hawautaki
 
Mpaka Leo sijawahi kuuona mchango wa Zanzibar kwenye muungano.... Tanganyika inaibeba sana Zenji....
 
Ndio maana wazanzibari wanataka ile Account ya pamoja ya Muungano ifanye kazi. Na vile vitu vyote vilivyoainishwa kama ni vya Muungano , mapato yagawanywe kama ilivyoaininisha Katiba. Venginevyo vunjeni huo Ukoloni munaouita Muungano. Hata huo Ukoloni huekeza kwenye koloni lake. Mfano mdogo Wajerumani ndio waliojenge njia ya Reli, ndio walioanzisha mashamba ya Mkonge, ndio walioanzisha kilimo cha Kahawa na mpaka leo ndio munayoringia, wajerumani ndio waliokifanyia structure hicho Kiswahili chetu kikawa kinaandikwa kwa herufi za kilatin. Sasa sisi huu unaitwa Muungano kwa Muda wa miaka hii 56 kuna kipi Zanzibar cha kukumbukwa kilicholetwa na huu unaoitwa Muungano? Hata ukimuona Mzanzibari anatetea Muungano, basi aidha kapewa cheo Bara na anteta maslahi yake na familia yake lakini sio ya Wazanzibari, na huo ndio ukweli mpaka dunia itamalizika
 
Kwanini mmekataliwa kuwa mwanachama wa FIFA
Wanadai wana kiti UN [emoji28][emoji28] wakati UN inatumbalika Tanzania kama member hakuna Zanzibar sasa sijajua hicho kiti kinawasaidia nini


Hawa watu ni wabishi na wapumbavu na hakuna mtu wa bara anayeetaka muungano ni viongozi wachache wenye manufaa yao huko kwao
 
Nilianza kuwa na mashaka pale aliposema Serikali itanunua meli 8 za uvuvi 4 Tanganyika na 4 Zanzibar, hii hapana aisee, Serikali ya muungano yaan tulipe kodi sisi wao wachukue meli 4,Mama Samia nchi itakushinda
Kwani wao hawalipi TRA, tumieni akili kidogo
 
Mnalalamika Zanzibar haina mchango wowote kwenye Muungano,ila AJABU NI KWAMBA WAZANZIBARI WAKITAKA KUJIONDOA KWENYR HUO MUUNGANO MNATUMIA HADI MITUTU KUHAKIKISHA HAWAONDOKI.

CCM na viongozi wa serikali wanaotoka Bara akili zao si timamu!
Wanasiasa ndio wanaushikilia Muungano kwa sababu ambazo pengine raia hatuzijui

Sisi raia tukiulizwa hata leo hatutaki Muungano

Kwahiyo msijifariji eti tunawahitaji sana, binafsi siwahitaji wazanzibar
 
Mama ashasema yeye na JPM ni wamoja.. Hivyo ameiga ile tabia ya kutofata sheria kwenye maamuzi yake... Ukiona hata Mwinyi ndio kama makamu wa Rais , wakati yeye ni wazinzabar, wakati hata kwenye line up ya uongozi wa uraisi wa JMT , yeye hayumo... Kwenye hotuba yake bungeni alivunja protocol, akaanza kumtaja Raisi wa Zanzibar , kabla ya makamu wa rais... Analeta mambo ya kimakunduchi .. aache siyo vizuri..
 
Tupe mfano wa msaada walioomba kwa siku za hivi karibuni
 
Muungano hauna faida Kwa watanganyika. Faida ipo Kwa wazanzibar tuu
Na siku tukisema wabara tujitoe hao jamaa sijui kama watakubali kirahisi au wanaweza kudai fidia UN utadhani ni ndoa ya binadamu
 
Muungano huu hauna faida kwa watanganyika. Unawafaidisha wazanzibari tu.

Anayebisha anyooshe mkono juu, au hata afanye kama anajikuna. Halafu alete faida moja tu ambayo mtanganyika anaipata.

Sasa kwanini munaung'ang'ania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…