Nilivyoona furaha ya wajumbe wa ZNZ waliotoka CAF na kusikia maoni yao walipohojiwa na waandishi wa habari, bila shaka ndugu zetu wazanzibari muungano hawautaki ila wamebanwa na wapo katika muungano kwa kushurutishwa.
Kwa wazanzibari kwao kuwa mwanachama wa CAF na kisha FIFA wakifanikiwa itakua ni ushindi mkubwa sana katika kudai sovereignty yao.
Kutokana na mazingira na kauli mbalimbali za viongozi wao wa upinzani na chama tawala, bila shaka Tanganyika tunawahitaji zaidi Zanzibar kuliko wao wanavyotuhitaji. Nimetembelea ZNZ zaidi ya mara kumi, wazanzibari muungano hawautaki. wanaosema wanautaka muungano wanadhihirisha vinywani tu ili kuungamkono msimamo wa chama chao CCM ila na wao ndani ya mioyo yao msimamo wao ni tofauti, hawataki kuonekana wasaliti.
Naamini uhuru wa kutambulika ktk michezo kama nchi huru ni ushindi na hatua kubwa kwa wazanzibari. Sasa wanajipa moyo kupata uhuru wa kisiasa, kukiwa na tume huru ya kusimamia uchaguzi na demokrasia ya kweli bila kutumia nguvu za kijeshi, wakiulizwa kuhusu muungano bila shaka ndio utakua mwisho.