Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
SMZ INAVYONUFAIKA NA MIKOPO, MISAADA NA DHAMANA KUPITIA SJMT
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Zanzibar inanufaika na fedha zitolewazo na Wadau wa maendeleo kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT).
Mhe. Khamis amesema hayo bungeni jijini Dodoma tarehe 9 Aprili, 2025 wakati akijibu swali la Mhe. Bakar Hamad Bakar (Baraza la Wawakilshi) aliyetaka kujua kwa kiasi gani Zanzibar inanufaika na fedha zitolewazo na Wadau wa maendeleo kupitia Serikali ya Muungano kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Akiendelea kujibu swali hilo, Mhe. Khamis ameeleza kuwa kupitia fedha hizo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kushirikiana na SJMT imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mhe. Khamis Hamza Khamis Ametaja miradi iliyotekelezwa kuwa ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume Pemba, Barabara ya Tunguu hadi Makunduchi, Chakechake hadi Wete kupitia kwa Binti Abeid na ujenzi wa Skuli, Hosptali na Masoko.
Mhe. Khamis Hamza Khamis Amesema miradi inayotekelezwa Zanzibar imewasaidia wananchi wa pande zote mbili za Muungano kushiriki na kuinua hali zao za kiuchumi pamoja na kuongeza ajira kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
”Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada Sura 134 imeweka utaratibu wa namna SMZ inavyopaswa kunufaika na mikopo, dhamana na misaada kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” Mhe. Khamis Hamza Khamis