Zanzibar Insurance Company kukataza wageni wasio na Bima kuingia Zanzibar ni kukiuka Katiba ya Nchi. Wanasheria wa serikali kwanini mnaruhusu haya?

Zanzibar Insurance Company kukataza wageni wasio na Bima kuingia Zanzibar ni kukiuka Katiba ya Nchi. Wanasheria wa serikali kwanini mnaruhusu haya?

Zanzibar ni nchi au mkoa au wilaya??
Wanaamuq mambo kwa mamlaka gani?
 
Nadhani kuna watu wana matamanio yaliyopitiliza. Najiuliza kama hawa wazanzibari wamefanya utafiti kwanza kabla ya kutoa tamko.!! 😳

Kwanza: uingiaji wa wageni ni suala linalodhibitiwa na Idara ya uhamiaji ambayo ni ya muungano. Je, Zanzibar inataka kujipangia mambo yake nje ya muungano?
Pili: Nijuavyo watalii wote huko watokako huwa wanabanwa na kipengele cha kuwa na bima ya afya kwa wasafiri, kigezo kinacho tekelezwa wakati wa kununua tiketi na ni makampuni ya bima ya nchi zao yanayoshughulikia suala hili. Je Zanzibar wana mkataba na hayo makampuni ya nje yanayotoa bima ya afya ili wageni wasitozwe mara mbili?

Tatu: Wageni wanaokuja Zanzibar wanapata visa ya JMT ambayo haijaweka kigezo cha mgeni kuwa na bima zaidi ya ile aliyokata nchini mwake, Je Zanzibar inajitenga rasmi na muungano ?

Nne: Imetangazwa kuwa ndege ya Air Tanzania inayofanya safari kati ya Dar es salaam na Dubai italazimika au kuanzia/kupita Zanzibar wakati wa kwenda na kurudi, Je hii ina tafsiri gani? Kwamba wanaokwenda Dubai ni wazanzibari tu au ndio maandalizi ya kununua ndege za Zanzibar? au kati ya hizo zilizonunuliwa kuna mgawanyo wa kuanzisha Zanzibar Air ????:AYOOO:🤔😎:3Dance::ClapHD:
 
Back
Top Bottom