Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Japo fani ya sheria ni fani moja simple sana, ndani ya sheria kuna sheria fulani fulani ni ngumu sana kwa mawakili.
Miongoni mwa sheria ngumu ni Criminal Law, Land Law, Law of evidence, Constitutional law na Public International Law.
Kwa upande wa sheria ya katiba, constitutional Law, Watanzania ni wa hurumiwa tuu, Mungu Saidia, sio serikali, sio Bunge wala Mahakama zetu zinafuata dhima ya mtunga katiba, ndio maana serikali yetu inatunga miswada batili ya sheria inayokwenda kinyume na katiba, Bunge linatunga sheria batili, Mahakama Kuu inabatilisha, sheria hizo batili, Mahakama ya Rufaa inakubalia na Mahakama Kuu kuhusu ubatili, kisha inajifunga mikono kwa kunawa mikono kujiosha kama Pilato alipomhukumu Mwana wa Adamu, kifo msalabani na inazirudisha Bungeni, Bunge lile lile lililotunga batili, at ndio limebembelezwa kuuondoa huo ubatili, matokeo yake ubatili huo upo mpaka leo ndani ya katiba yetu na ndani ya sheria yetu ya uchaguzi na hadi hii sheria mpya ya uchaguzi ni batili!.
Kwa upande wa International law, kuna miungano ya aina kuu 3
1. Muungano wa Total Union
2. Muungano wa Federation
3. Muungano wa Confederation
Aina ya muungano wetu wa URT ni muungano unique wa mseto wa Total Union kwa upande mmoja nchi mbili za (Tanganyika na Zanzibar ) zimeungana kuunda taifa moja URT. Nchi zote mbili zimekufa.
Kwa upande wa pili ni muungano wa Federation ya Tanzania na (Zanzibar).
kuunda taifa la federal lenye independent states ndani yake kama ilivyo USA, USSR、Yogoslavia etc
Kiukweli kabisa Muungano wetu kimataifa ni muungano wa unitary, hauna utata wowote, muungano wetu ni Muungano wa Union ya nchi mbili zimeungana, zote zikapoteza sovereignty zake kwa kuzikabidhi kwa nchi moja ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kimataifa,Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika, na Tanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani.
Kizungumkuti cha muungano wetu ni Tanzania ndani ya Muungano, Muungano wetu ni wa federation yenye washirika wawili, katiba mbili, Marais wawili, mabunge mawili, mshirika mmoja ndie nchi mwenye sovereignty na mshirika wa pili sio nchi, hana sovereignty, ila kwenye katiba yake anajiita ni nchi, katiba ya mshirika mwingine haiitambui katiba ya mshirika mwenzake!, mambo ni shaghalabaghala!.
Mshirika ambaye sio nchi, akajiunga na OIC, hivyo kuonekana kama ni Tanzania ndio imejiunga na OIC, Bunge la mshirika mmoja likakasirika na kumlazimisha mshirika huyo ajitoe OIC, kwa ahadi ya Tanzania itajiunga, kumbe ni danganya toto!.
Sasa baadhi ya Wanzanzibari wanatamani kujiunga na OIC.
Kwa vile Zanzibar sio nchi, haina sovereignty, has no capacity to contract an international treaty, hivyo mikataba yote ya kimataifa ya Zanzibar, inaingiwa na JMT kwa niaba ya Zanzibar, na ikitokea Zanzibar ikashindwa kulipa deni, anayelipa ni JMT. Hili la mkataba kama wa DP World nimelizungumza humu
Hebu msikie Mzanzibari hiyu akililia OIC
Sasa kama Tanzania ambayo ni nchi, ikaingia mkataba wa kimataifa na Dubai ambayo sii nchi, ukaletwa Bungeni na kuridhiwa na Bunge letu, then kwanini Zanzibar inazuiwa kuingia mikataba ya kimataifa wakati mwenzake Dubai anaingia?.
Kama kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, Zanzibar inajiita ni nchi lakini sio nchi!, ila kama kweli Zanzibar ni nchi, haihitaji ruhusa ya mtu yeyote kujinga OIC, wala haihitaji udhamini wa mtu yeyote kuingia mikataba ya kimataifa!.
Ndio maana wakati wa mjadala wa DP World na Bandari zetu, nilisema mkataba ule umetusaidia sana kuujua ukilaza wa wanasheria wetu na serikali yetu, Bunge letu na Mahakama yetu, kuridhia mkataba wa an entity which has no the capacity to contract, nikawashauri Zanzibar to take that advantage kuikata minyororo inayowazuia kuifanya Zanzibar iwe a free port.
Kama kwa Dubai Tumeweza, Why not Zanzibar?.
Paskali

Kwa vile the status of Zanzibar ndani ya Muungano ni sawa sawa kabisa na the status of Dubai ndani ya UAE, Dubai imepewa special status, inaweza kuingia mikataba ya kimataifa ya kibiashara.