Kama Zanzibar ni nchi au si Nchi hayo ni yenu huko bara ,ila wenyewe wanasema Zanzibar ni nchi mwenye wivu ajinyonge.
La pili naona mmetoka roho kwa matrekta 50 basi hayo ni kianzio zipo ahadi kibao ambazo Zanzibar imeahidiwa.
La Tatu mkuu wenu Kikwete juzi alijisifu kwa misaada waliyotoa watu wengine akisema serikali yake imeleta maendeleo basi hayo matrekta 50 yatampa tena mdomo mwengine wa kusifu maendeleo yanayoletwa na serikali yake.
Weka kando hilo maana naona hii topiki imechanganywa wakati kuna mambo mawili tofauti hapa. Niwaulize wanaJF hivi kama mnafahamu maendeleo nitawapa haya mambo ambayo ikiwa kati yenu kuna mtu alikuwepo Zanzibar kati ya kwenye mwaka wa 1980 hadi 1989 ataweza kuona tofauti .
Tuangalie Maendeleo yaliokuwepo Zanzibar natumai hata Tanganyika yalikuwepo maana nakumbuka lile bulga la saa nne kwa waliosoma Tanga wanaujua uji huo.
Tuangalie maendeleo yalikuwapo leo yako wapi??????
1. Tulikuwa na viwanda mbali mbali kama vile cha sukari, viatu, maziwa, sigara na viwanda vidogo vidogo lakini leo vyote leo haviko;
2. Tulikuwa na meli za kifahari kama vile MV. Mapinduzi, MV. Uhuru, MV. Ukombozi leo zimekuwa mzigo kwa Serikali na hutamani hata kupanda kwa girisi iliyojaa na wakati mwingi huwa hazifanyi kazi;
3. Skuli tulipokuwa tunasoma tulikuwa tunapewa vitabu mbali mbali vya kufanya marejeo nyumbani kama Modern Biology, Physics, Chemistry, Geography ...nk. Pia tulikuwa tunakaa kwenye desk kila Mwanafunzi lake lakini leo wengi wanakaa chini;
4. Skuli tulikuwa tunatumia vifaa vya maabara vipya kutoka Uingereza kama vile Bursen burner, test tube, beakers, measuring flasks ...nk lakini leo skuli nyingi hazina vifaa hivyo;
5. Hospitali ukipelekwa kwanza unapewa cheti lakini leo unaambiwa ukanunue buku nje utafikiri unakwenda kusoma. Pia baada kwisha kuonana na Daktari unakwenda kuchukua dawa ambazo zote huwepo bila matatizo lakini leo inabidi ukanunue nje kwa Utapoa;
6. Nyumba tuliokuwa tunakaa ilikuwa ukifungua maji basi lazima ukamate kikombe kwa uangalifu au kikombe hicho kinaweza kukutoka kwa pressure ya maji lakini leo tokea mwaka 1994 hadi leo hakuna maji yaliyotoka;
7. Rais wa Zanzibar alikuwa pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini leo hata cheo chake hatukijui ni kipi maana tumeambiwa kuwa si nchi. Sasa utakuwa Rais usiokuwa na nchi?
8. Wa-Zanzibari ilikuwa ni aibu kupita njiani kuomba lakini leo limekuwa jambo la kawaida kutokana na dhiki za maisha kutokana na dudu la TRA kutukaba rohoni.
Sasa nawauliza pamoja na huyu mmachinga wa Chalinze Mkwere Kikwete apime au ayaone hayo yaliopo hapo na kama anahitaji ushahidi awaulize CCM wenziwe waliopo Zanzibar kama hayo ni ya kweli au ni propaganda ? Je hayo ni maendeleo au si maendeleo ? Hayo ndio yanayohitajika ili Serikali na yeye Kikwete kama Kiongozi wa au Raisi wa Tanzania na Mwenyekiti wa AU basi ndio maendeleo ya kujisifia linganisha barabara na hayo hapo yepi ni muhimu ? Na hasa ilivyokuwa ya juu yote yamefanywa na serikali kama matunda ya mapinduzi ni hayo yaliopo juu na si haya maendeleo anayoyasifu mlinda mapinduzi mpya Mh.Kikwete ,ni lazima akae afikiri sana sio anakwenda Pemba na Unguja na kupandwa na jazba. WaZanzibari wanajua lipi bichi na lipi limeiva ,maendeleo ya Zanzibar chini ya awamu zote tatu za uongozi Tanzania ni sifuri,hivi Kikwete na kwenda kwake kote katika safari zake za utalii kutembea hajaona maendeleo ya Nchi nyingine au anakenua tu na kupiga miruzi anapoona vya watu vinang'ara.
Kikwete amewakosea adabu watu wa Zanzibar kwa kuwambia ni walevi wa tende kwani na kusema hakutapatikana uongozi unaotokana na ridhaa za wananchi huko ni kutokuheshimiana ,maana unaposema uongozi wa kuiongoza Zanzibar kwa upinzani itawachukua muda mrefu au usipatikane kabisa huko ni kuvuka mipaka ya utawala bora ukichanganya na demokrasia yake,ingawa huo uongozi bora haupo lakini inabidi ichomekewe hivyo hivyo. Kwenda kuwasifia watu tangi la maji wakati maji yenyewe hakuna huko ni kuwadharau na kuwafanya kama ni kuwadanganya watoto wadogo unaotaka kuwakimbia.
Zanzibar will prevail even under mkoloni mweusi.