Zanzibar kunyimwa uanachama wa FIFA na CAF ni chuki kisiasa au kukosa vigezo?

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Zanzibar sio jimbo la Tanzania ila ni nchi iliyopo kwenye muungano, natamani sana siku moja nione ikicheza kimataifa na hakika watafika mbali.

Kwanini haya mashirikisho ya kimataifa yanawanyima uanachama? Hawana vigezo vya kuwa mwanachama au kwa sababu wapo kwenye muungano na Tanzania bara?

Kuna nchi zipo kwenye muungano na bado wana uanachama wa FIFA na shirikisho husika bara walilopo, mf.

1. Wales
2. England
3. Ireland
4. Hong Kong
5. Kosovo n.k.

Ni nini kinaikwamisha Zanzibar kupewa uanachama kamili ilihali ngazi ya club bingwa Afrika wanapeleka timu, hii imekaaje wataalamu wa soka?
 
Tunaposema Wazanzibari Hatutaki Muungano mutuelewe Watanganyika.
 
Ukibebwa, basi jitahidi ujishikilie! Zanzibar wamebebwa na CAF kwa kupewa nafasi mbili za klabu zao kushiriki CAF Champions League a Confederation Cup. Lakini hawa jamaa huwa wanaishia raundi ya awali, na wakijitahidi sana wanaishia raundi ya kwanza. Sasa hapo inakuwa ni vigumu hata kuweza kuishawishi CAF itoe nafasi hiyo kwa ngazi ya timu za taifa
 
Katiba Mbovu ya Tanganyika ndio maana Masheikh wako ndani.One day yes.
 
Zanzibar sio jimbo la Tanzania ila ni nchi iliyopo kwenye muungano, natamani sana siku moja nione ikicheza kimataifa na hakika watafika mbali.

Kwanini haya mashirikisho ya kimataifa yanawanyima uanachama? Hawana vigezo vya kuwa mwanachama au kwa sababu wapo kwenye muungano na Tanzania bara?

Kuna nchi zipo kwenye muungano na bado wana uanachama wa FIFA na shirikisho husika bara walilopo, mf.

1. Wales
2. England
3. Iriland
4. Hong Kong
5. Kosovo n.k.

Ni nini kinaikwamisha Zanzibar kupewa uanachama kamili ilihali ngazi ya club bingwa Afrika wanapeleka timu,hii imekaaje wataalamu wa soka?
Tunafanyia utaratibu mpya muungano wetu ili mambo kama haya yapate utatuzi, Zanzibar ni nchi kama nchi nyingine zilizopo kwenye muungano, na itafika wakati kutakuwa na uchaguzi mkuu wa uraisi wa Zantania na ule wa Tanganyika.
Kazi iendelee.
 
Ukibebwa, basi jitahidi ujishikilie! Zanzibar wamebebwa na CAF kwa kupewa nafasi mbili za klabu zao kushiriki CAF Champions League a Confederation Cup. Lakini hawa jamaa huwa wanaishia raundi ya awali, na wakijitahidi sana wanaishia raundi ya kwanza. Sasa hapo inakuwa ni vigumu hata kuweza kuishawishi CAF itoe nafasi hiyo kwa ngazi ya timu za taifa
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Zanzibar kimpira wako juu kuliko huku bara.
 
zanzibar sio nchi sema wanalazimisha waonekane ni nchi, wasapoti serikali tatu ili wawe na mamlaka kanili ya nchi yao itambulike kimataifa au wajitoe kabisa kwenye muungano watuachie tanganyika yetu.
 
Tunaposema Wazanzibari Hatutaki Muungano mutuelewe Watanganyika.
Niko pamoja na nyie kwenye ishu ya muungano
Ukibebwa, basi jitahidi ujishikilie! Zanzibar wamebebwa na CAF kwa kupewa nafasi mbili za klabu zao kushiriki CAF Champions League a Confederation Cup. Lakini hawa jamaa huwa wanaishia raundi ya awali, na wakijitahidi sana wanaishia raundi ya kwanza. Sasa hapo inakuwa ni vigumu hata kuweza kuishawishi CAF itoe nafasi hiyo kwa ngazi ya timu za taifa
Vipi Comoro ya 2010 unaikumbuka? Vip na ya sasa?
 
Back
Top Bottom