Mhe. Mwinyi ni mkuu wa kitongoji.? Em nieleweshe bossZanzibar sio nchi
Tusubiri majibu yakeAu tuseme ni mkuu wa mkoa wa Z'bar🤣🤣
Tunafanyia utaratibu mpya muungano wetu ili mambo kama haya yapate utatuzi, Zanzibar ni nchi kama nchi nyingine zilizopo kwenye muungano, na itafika wakati kutakuwa na uchaguzi mkuu wa uraisi wa Zantania na ule wa Tanganyika.Zanzibar sio jimbo la Tanzania ila ni nchi iliyopo kwenye muungano, natamani sana siku moja nione ikicheza kimataifa na hakika watafika mbali.
Kwanini haya mashirikisho ya kimataifa yanawanyima uanachama? Hawana vigezo vya kuwa mwanachama au kwa sababu wapo kwenye muungano na Tanzania bara?
Kuna nchi zipo kwenye muungano na bado wana uanachama wa FIFA na shirikisho husika bara walilopo, mf.
1. Wales
2. England
3. Iriland
4. Hong Kong
5. Kosovo n.k.
Ni nini kinaikwamisha Zanzibar kupewa uanachama kamili ilihali ngazi ya club bingwa Afrika wanapeleka timu,hii imekaaje wataalamu wa soka?
Tatizo kubwa ni wazanzibar wenyewe kushindwa kujitoa kwny huu muungano wa kipuuz
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.Ukibebwa, basi jitahidi ujishikilie! Zanzibar wamebebwa na CAF kwa kupewa nafasi mbili za klabu zao kushiriki CAF Champions League a Confederation Cup. Lakini hawa jamaa huwa wanaishia raundi ya awali, na wakijitahidi sana wanaishia raundi ya kwanza. Sasa hapo inakuwa ni vigumu hata kuweza kuishawishi CAF itoe nafasi hiyo kwa ngazi ya timu za taifa
Niko pamoja na nyie kwenye ishu ya muunganoTunaposema Wazanzibari Hatutaki Muungano mutuelewe Watanganyika.
Vipi Comoro ya 2010 unaikumbuka? Vip na ya sasa?Ukibebwa, basi jitahidi ujishikilie! Zanzibar wamebebwa na CAF kwa kupewa nafasi mbili za klabu zao kushiriki CAF Champions League a Confederation Cup. Lakini hawa jamaa huwa wanaishia raundi ya awali, na wakijitahidi sana wanaishia raundi ya kwanza. Sasa hapo inakuwa ni vigumu hata kuweza kuishawishi CAF itoe nafasi hiyo kwa ngazi ya timu za taifa
Kama Zanzibar sio nchi kwa nini wana Rais, Bendera, jeshi, bunge, katiba, baraza la mawaziri, wimbo wa taifa na mipaka inayotambulika ?Zanzibar sio nchi.Tanzania ndio nchi