Zanzibar Ligi yasimama kupisha mfungo wa Ramadhan

Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Kuu Zanzibar (@zffzanzibar), Hashim Salum ametangaza kuwa Ligi Kuu ya Zanzibar itasimama kwa muda wa mwezi mmoja kupisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuanzia ulioanza leo.
Ligi hiyo inatarajia kurejea Mei 6, 2023.

Chanzo: East Africa TV

Wangejua wachezaji na mashabiki wanakula usiku kucha kama viwavi hata wasinge sitisha ligi.
 
Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Kuu Zanzibar (@zffzanzibar), Hashim Salum ametangaza kuwa Ligi Kuu ya Zanzibar itasimama kwa muda wa mwezi mmoja kupisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuanzia ulioanza leo.
Ligi hiyo inatarajia kurejea Mei 6, 2023.

Chanzo: East Africa TV
Hiyo wanajua wenyewe siyo ligi. FIFA inaitambua?
 
Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Kuu Zanzibar (@zffzanzibar), Hashim Salum ametangaza kuwa Ligi Kuu ya Zanzibar itasimama kwa muda wa mwezi mmoja kupisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuanzia ulioanza leo.
Ligi hiyo inatarajia kurejea Mei 6, 2023.

Chanzo: East Africa TV
Sehemu kubwa sana ya wakazi wa Tanzania Visiwani ni waumini wa dini ya Kiislamu. Kwa hiyo basi Kila ufikapo mwezi huu wa Ramadhan, na kutokana na umuhimu wake katika dini hii ni lazima tu utaathiri shughuli zote za kiuchumi, kijamii na hata pia zile za kiutamaduni ikijumuisha shughuli za michezo.

Hili jambo la kawaida kwa kila nchi yenye idadi kubwa ya Waislamu. Na pia hata jamii nyingi hapa nchini zenye idadi kubwa ya waumini wa dini hii jambo hili halijifichi kabisa. Naombeni tuchukuliane kwa jinsi tulivyo na jinsi tunavyojitambua kutoka na imani zetu.

Sidhani kama kuna umuhimu wowote ule wa kujali endapo jamii fulani isiyofungamana na imani yako wakifanya yale wapaswayo kuyafanya kuendana na imani yao. Sidhani kama mtu atapungukiwa na kitu chochote kile endapo ligi ya Zanzibar ikipisha kipindi cha mfungo, wakati wadau ambao ni waaumini wakiadhimisha kwa dhati na uaminifu mkubwa mojawapo ya nguzo kuu ya dini yao.
 
Zanzibar ni kupe tu kwa Tanganyika. Ingekuwa ni nchi, isingekuwa tegemezi kwa Tanganyika kwa miaka mingi.

Wakiambiwa wajitegemee kama nchi kwa 100%, hawataki. Maana wanajua fika watakosa mambo mengi mazuri kutoka Tanganyika.
Huu ni ukweli mtupu.
 
Sehemu kubwa sana ya wakazi wa Tanzania Visiwani ni waumini wa dini ya Kiislamu. Kwa hiyo basi Kila ufikapo mwezi huu wa Ramadhan, na kutokana na umuhimu wake katika dini hii ni lazima tu utaathiri shughuli zote za kiuchumi, kijamii na hata pia zile za kiutamaduni ikijumuisha shughuli za michezo.

Hili jambo la kawaida kwa kila nchi yenye idadi kubwa ya Waislamu. Na pia hata jamii nyingi hapa nchini zenye idadi kubwa ya waumini wa dini hii jambo hili halijifichi kabisa. Naombeni tuchukuliane kwa jinsi tulivyo na jinsi tunavyojitambua kutoka na imani zetu.

Sidhani kama kuna umuhimu wowote ule wa kujali endapo jamii fulani isiyofungamana na imani yako wakifanya yale wapaswayo kuyafanya kuendana na imani yao. Sidhani kama mtu atapungukiwa na kitu chochote kile endapo ligi ya Zanzibar ikipisha kipindi cha mfungo, wakati wadau ambao ni waaumini wakiadhimisha kwa dhati na uaminifu mkubwa mojawapo ya nguzo kuu ya dini yao.
Wanapisha eating festival, sherehe za kula kupita maelezo
 
Mkuu jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Hii ni mojawapo ya nguzo za dini ya Kiisilamu, unathubutuje hata kuweza kuiita kama "karamu ya kunywa na kula, na tena ukachomekea na neno la kupitiliza yaani ulafi"!?

Ogopa sana Mola wako, na chunga sana kauli zako, hasa pale jambo la kiimani likifanywa na waja wake na wewe kulifanyia kejeli. Wanasema mdomo uliponza kichwa, ila mimi ninasema andiko lako linaweza kuwa sehemu ya hukumu yako kwa yule ayaonaye mambo ya sirini.
 
Ni eating festival waislamu wanakula na kunywa vizuri kuliko miezi mingine

Kiufupi ni karamu ya kula na kunywa
 
Mapumziko ya Pasaka na X-mass yapo wewe umezungumzia mapumziko ya Kwaresma.
Kwani mapumziko hayo yanawahusu nini waislamu wa huko walio wengi
Hilo ni tatizo.
Kwani huku bara hakuna wachezaji waislamu ? Mbona mapumziko hayo hakuna
 
Naona msio kua waislam mnaumizwa sana na kila kitu kinachofanywa na waislam hata kama haki waathiri kwa namna yeyote ile. Mfano mdogo tu ni kwamba Ligi imesimamishwa Zanzibar, wamesimamisha Wazanzibar wenyew, wapo huko Kwao Zanzibar na wewe upo kwenu popote ulipo nje ya Zanzibar kusimamisha kwao au kutokusimamisha hakukuathir ww hata kama usingekuepo huko Zanizbar, ila tu kwavile wamefanya kqa ajil ya kutekeleza ibada Ya Uislam basi nyinyi mnaumia sana na mnalalamika.
Poleni sana kwanza.
Lkn pia hili Allah alishalisema ktk Kitabu kitukufu.
Laa tardhwa ankal yahud wa nnasara hatta tattabia millatahum.
 
Back
Top Bottom