GE2025 Zanzibar: Magari yenye plate number za Mwinyi 2025 na SSH 2530 zakamatwa

GE2025 Zanzibar: Magari yenye plate number za Mwinyi 2025 na SSH 2530 zakamatwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani pamoja na mamlaka nyingine zimefanikiwa kukamata namba zisizotambulika na mamlaka husika zilizokuwa zikifungwa katika eneo la kibati cha namba (Plate number) kwenye vyombo vya moto.

Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mkurugenzi wa Upelelezj na Makosa ya jinai Zanzibar Naibu Kamishna wa Polisi Zubeir Chembera amesema Mnamo tarehe 25/07/2025 hadi 04/08/2025 Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani(ZARTSA) na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), wamefanya operesheni ya pamoja ya siku kumi (10) katika maeneo mbalimbali ya Mikoa ya Unguja.

Amesema Katika Operesheni hio Jumla ya makosa 2,641 yalikamatwa ambapo Gari zilikuwa ni 814 na pikipiki zilikuwa ni 1,827 pamoja na kutoza Tsh. 230,618,750/= kama Tozo kwa makosa hayo.

Aidha amesema katika Operesheni hiyo pia yalikamatwa magari yaliyofunga namba zisizotambulika na Mamlaka za usajili kama SSH 25-30, MWINYI 2530, TAMBA NA AMEIR URAIS 2025-2023, kufunga taa za vimulimuli na baadhi ya magari kutumia nambari za Tanzania Bara bila ya kibali kutoka Mamlaka husika, vitendo hivi ni makosa kwa mujibu wa sheria ya Usafiri Barabarani ya Zanzibar.

Screenshot 2025-09-11 223525.png
 
Huku bara polisi wanatuambia hadi ukiona gari ya aina hiyo ndio ukatoe taarifa polisi, hii maana yake wao hawajakutana na hayo magari.
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Back
Top Bottom