You are very right! Uhai hauna spare!Jiponye nafs yako...!!! Uhai wa watu wengi haujawah kuwa justified na mtu mmoja haijalishi ana nguvu Kias gan , never ever , , tutabak kulaumiana tuu huku wenzetu wakishuka kaburini..... Uhai wa mtu mmoja mmoja ndo Jambo la kuchangamkia , tuna roho moja tuu na haina spea ikienda imeenda..... Wahindi wamelijua hili mapema Sana
SaafiNobody Can Stop Reggae.
Ila hapa napata ukakasi kwamba huenda kuna jambo limejificha.Chama cha ACT kujitoa kimbelembele kutangaza hili wakati huyu mtu ni makamu wa Rais ambaye yupo kwenye mamlaka za juu ambazo zingeweza kulisemea kwa uzito wake.Kuna jambo.TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19
Chama cha ACT Wazalendo kinawajuilisha wanachama wake, Wazanzibari, pamoja na umma wa Watanzania, kuwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe, Bi Awena, pamoja na Wasaidizi wake kadhaa wa karibu, wamethibitika kupata maambukizi ya Virusi vya Covid 19 baada ya kufanyiwa vipimo.
Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi Madaktari walimshauri Maalim Seif kuwa ni vyema awepo chini ya uangalizi maalumu katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu dhidi ya Korona. Hivyo basi, tangu juzi Ijumaa jioni, Maalim Seif alipumzishwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar, ambako anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa Madaktari.
Tunapenda kuchukua nafasi hii kuujulisha umma kuwa hali ya Maalim Seif pamoja na mkewe zinaendelea vyema kabisa, Viongozi wenzake pamoja na Wanafamilia wamekuwa na mawasiliano naye ya kawaida kila siku.
ACT Wazalendo tunawaomba wanachama wetu, Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kumuombea dua Maalim Seif katika kipindi hiki ambacho amepumzishwa ili aweze kupona kwa haraka na arudi kuendelea na majukumu yake. Pia, tunarejea wito wetu kwa Watanzania wote kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya ugonjwa huu.
Ado Shaibu,
Katibu Mkuu,
ACT Wazalendo
31 Januari, 2021.
Chanzo: TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19
MY TAKE:
Hivi karibu Januari 14, 2021 Seif alitembela Chato. Je, Watu aliyokutana nao tahadhari?
Soma: Rais Magufuli: Maalim Seif ni Kiongozi kweli, aliacha 'interest' zake na kutanguliza za Wazanzibari
Kwani hata Maalim Seif kanaumwa?Haipo ndio.kama ipo wapo wapi?
Ila hapa napata ukakasi kwamba huenda kuna jambo limejificha.Chama cha ACT kujitoa kimbelembele kutangaza hili wakati huyu mtu ni makamu wa Rais ambaye yupo kwenye mamlaka za juu ambazo zingeweza kulisemea kwa uzito wake.Kuna jambo.
uanze wewe kwanza,Network ikamate mpaka huku bara kwa wale wakubwa zaidi. wasife ila wahenyeshwe tu mpaka waseme coona ipo kwelikweli
Kwani wauaji tbccm wao wamesemajiChama cha ACT Wazalendo kimethibitsha kuwa kiongoz wake MAALIM SEIF SHARIF HAMAD ANA Corona...pamoja na wasaidizi wake wa jirani..CREDIT: eatv
Kwani hata Maalim Seif kanaumwa?
Mwinyi leo usiku akakeshe na mgonjwa hapo hospital kama ishara ya kuliponya taifa.
Upo sahihi.Malimao ya nini wakati Tanzania hakuna Corona?
Corona haipo. Corona ilikwisha. Aah aah ipo kidogo tu.
Kwamba ACT wametangaza, pana mijamaa ya chama fulani itakuwa imeumia kweri kweri.
Au nasema uongo ndugu zangu?
Lini utatabiri Tanzania kuingia lock down?.
Kwahiyo zilishapita na hivyo Jiwe is safe?Incubation period is between 5-6 days.