Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Zanzibar Mental Health Support Organization imeanza kutekeleza Rasmi Mradi wa Elimu ya Afya ya Akili Mashuleni
Unguja, Zanzibar – 23 Januari 2025
Zanzibar Mental Health Support Organization (ZAMHSO) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya, imeanza kutekeleza rasmi mradi wa kutoa elimu ya afya ya akili mashuleni. Amabopo wameanza na Skuli ya Magufuli, Kwerekwe, Unguja, ambapo shughuli za mradi zimeanza mara moja, zikiwahusisha walimu, Wanafunzi, na wataalamu wa Afya ya Akili.
Mradi huu unalenga kuongeza uelewa wa changamoto za Afya ya Akili shuleni na kuimarisha ustawi wa wanafunzi kupitia elimu, ushauri nasaha, na mafunzo kwa walimu. Kwa kipindi cha miezi sita ijayo, ZAMHSO itatembelea shule mbalimbali kisiwani Unguja ili kufanikisha lengo hili.
Wakati wa uzinduzi huo, wanafunzi wa Kada ya Saikolojia wakishirikiana na wataalamu wa ZAMHSO walitoa elimu ya Afya ya Akili kwa wanafunzi wa Skuli ya Magufuli, huku walimu wakipata mafunzo maalum kutoka kwa wataalamu wa masuala ya saikolojia.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa ZAMHSO, Mwalimu wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Abdurahman Al-Sumait, na Mwanasaikolojia kutoka Hospitali ya Ampola Tasakhtaa, Zaituni Shabani Salum, alisema:
“Hali ya afya ya akili mashuleni bado ni changamoto kubwa. Wanafunzi wengi wanakabiliwa na matatizo ya kiakili yanayoathiri uwezo wao wa kujifunza na kufaulu. Kwa bahati mbaya, uelewa mdogo kuhusu afya ya akili umesababisha wengi wao kukosa msaada muhimu. Kupitia mradi huu, tunalenga kuleta mabadiliko kwa kuhakikisha kwamba wanafunzi, walimu, na hata wazazi wanapata elimu itakayowawezesha kuelewa changamoto hizi na kuchukua hatua zinazofaa.”
Aidha, Zaituni aliwahimiza walimu na jamii kwa ujumla kushirikiana katika kukuza ustawi wa wanafunzi, huku akielezea matumaini kwamba mradi huu utaleta athari chanya kubwa kwa jamii ya Zanzibar.
Katika tukio hilo, wawakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya, pamoja na Hospitali ya Afya ya Akili ya Kidongo Chekundu walikuwepo kutoa shukrani na kuunga mkono juhudi hizi za ZAMHSO.
Mradi huu wa miezi sita unategemea kuhitimishwa mwishoni mwa mwezi Juni, kabla ya kuendelea na awamu yake ya pili kisiwani Pemba kuanzia Agosti hadi Desemba.
Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu au jinsi ya kushirikiana, tafadhali wasiliana na:
Zanzibar Mental Health Support Organization (ZAMHSO).
Pia soma:
~ Zaituni Shabani Salum wa ZAMHSO: Elimu ya Afya ya Akili ni nguzo muhimu kwa kizazi chetu
~ ZAMHSO: Mradi wa Afya ya Akili Shuleni utaacha athari chanya na kuleta mabadiliko ya kudumu