Zanzibar: Msichana wa kazi abakwa na Boss wa Miaka 74, Polisi wadaiwa kupoteza Ushahidi

Zanzibar: Msichana wa kazi abakwa na Boss wa Miaka 74, Polisi wadaiwa kupoteza Ushahidi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
MSICHANA WA KAZI KABAKWA NA MZEE WA MIAKA 74 AMBAYE NI BOSS WAKE MKAZI WA BUBU, ZANZIBAR, POLISI WADAIWA KUPOTEZA KESI!

Mheshimiwa Rais Hussein Mwinyi aombwa Kuingilia kati sheria ifuate mkondo

Bubu, Zanzibar.

Mzee Sadalla Juma Sadalla mwenye umri wa miaka 74 mkazi wa Bubu, Zanzibar anakabiliwa na kosa la kumbaka msichana wake wa kazi ambaye yupo chini ya umri wa miaka 18 na kumuingilia kimapenzi kwwa nguvu, msichana huyo ambaye jina linaifadhiwa alifanikiwa kutoa riport kituo cha Polisi Bubu.

Lakini hadi leo polisi wanajaribu kuipotezea mbali kesi hiyo na Mtuhumiwa Bw. Sadalla Juma Sadalla amechiwa bila kufikishwa mahakamani.

Juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za kukomesha unyanyasaji wa kijinsi na ubakaji viisiwani hapa zinagonga mwamba kutokana na wenye tabia za ubakaji kama Bw. Sadalla Juma Sadalla kutopelekwa mahakamani na sheria ikachukua mkondo wake.

Wanaharakati wa kuzuwia vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia visiwani Zanzibar wanakilalamikia kituo cha Polisi Bubu kwa kumwachia huru mbakaji Sadalla Juma Sadalla.

Wamemuomba Mheshiwa Rais Hussein Alli Mwinyi kuingilia kati kesi hii ya ubakaji hili sheria ifuate mkondo wake, wanaharakati hao wamemtaja mtuhumiwa Bwana Sadallla Juma Sadallla kuwa ni mtu aliyetajwa mara nyingi katika matukio ya kuwangilia kwa nguvu au kuwabaka watoto wenye umri mdogo na matukio hayo anayafanya hapa Unguja na Dar es salaam.

Vyombo vya ulinzi na usalama vinaombwa kuhakikisha Bw.Sadalla Juma Sadalla anafikishwa mbele ya sheria na hasipewe nafasi ya kukimbia Zanzibar.
 
Chini ya miaka 18?! mzee kazingua, angekuwa kuanzia miaka 26 ningesema kajitakia kubakwa au yeye ndo kambaka mzee.
 
Huyo mtoto kwao wapii ?

Kama mtoto sio mzawa wa zenji bila shaka atakuwa hana mtetezii huko wa kumsimamia.

Na kama mzee sadala kayafanya hayo kwa watoto wa kiizenji basi bila shaka wanayamaliza nyumbani.

Wanaharakati wanapiga kelele weee huku wahusika wanayamaliza nyumbani.

Hiyo ndio zanzibar kesi nyingi huenda hivyo.
 
Huyo mtoto kwao wapii ?

Kama mtoto sio mzawa wa zenji bila shaka atakuwa hana mtetezii huko wa kumsimamia.

Na kama mzee sadala kayafanya hayo kwa watoto wa kiizenji basi bila shaka wanayamaliza nyumbani.

Wanaharakati wanapiga kelele weee huku wahusika wanayamaliza nyumbani.

Hiyo ndio zanzibar kesi nyingi huenda hivyo.
Nasikia huko zenji wanamichezo ya kutifuana mpaka tope, afu wanayamaliza nyumbani.
 
Wanaharakati hawakupiga kelele wakati mtoto wa chini ya miaka 18 ameajiriwa kitu ambacho kiko kinyume na Sheria, halafu wanaharakati kumbe hawakuwahi kureport maovu ya huyu awali maana kumbe anaendaga hadi Dar kuyafanya haya.sadala sasa amekuwa tishio .
 
Back
Top Bottom