Zanzibar: Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote wapita

Zanzibar: Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote wapita

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha Muswada wa Bima ya Afya kwa wote huku Serikali ikiahidi kuhakikisha mfuko huo unakwenda kutekeleza malengo yake ya kuwapatia Wananchi huduma za Afya kikamilifu kwa makundi yote.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dkt. Saada Mkuya alisema Wizara ya Fedha ndio yenye jukumu la kuhakikisha linatafuta fedha na kukusanya kwa ajili ya kuhudumia mfuko wa bima ya afya na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Mkuya alikuwa akijibu hoja za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochangia Muswada huo uliowasilishwa na Waziri wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui.

Alisema kuanza kazi kwa mfuko huo wa kiasi kikubwa kutasaidia kufanikisha malengo yake ya kutoa huduma za afya kwa ufanisi na kuwaridhisha Wananchi.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Riziki Pembe Juma alisema mfuko wa Bima ya Afya ni mkombozi kwa makundi yaliyopo pembezoni ikiwamo Wanawake, Watoto na watu wenye ulemavu kuona wanapata huduma za afya kwa uhakika zaidi.

Alisema kuwapo kwa Bima ya Afya kwa kiasi kikubwa itasaidia kuwepo kwa huduma bora za wajawazito na kupunguza vifo na hivyo kuyafikia malengo endelevu ya Dunia yanayosisitiza afya bora na kupunguza vifo kwa watoto.

Awali, Waziri wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui akitoa ufafanuzi wa huduma za Boa ya Afya alisema ndio njia pekee itakayowawezesha Wananchi wote yakiwamo makundi yasiyokuwa na uwezo kufaidika na huduma za Afya kikamilifu.

Alisema mfuko wa bima ya afya umekuja baada ya kubainika kwamba yapo makundi hayafaidiki na huduma za afya ikiwemo watu wenye kipato cha chini waliopo vijijini.

Chanzo: Habari Leo
 
Hela wakusanye kutoka wapi?wawe wawazi tu hela wanategemea walipa kodi watanganyika wawalipie bima zao.
 
Back
Top Bottom