Zanzibar na utalii inapitia wakati mgumu. Tuiombee Trump asiendelee kuchochea vita

theprogrammer C++

Senior Member
Joined
May 17, 2013
Posts
150
Reaction score
385
Mahoteli ni matupuuu,hata zile budget hostels. Utalii unayoyoma kwa kasi aisee.

Uchumi wa Zanzibar ni utalii naa utalii wa Zanzibar umeshambuliwa na Serikali na global instability especially middle east. Ndege zote za watalii wanokuja Zanzibar chanzo kikubwa ni middle east. Ukijumlisha na tighter investments conditions na large government ongoing projects which needs constant cash flow,combination hizi zote zinabana sana .

Hali ikiendelea hivi, biashara ndogo za utalii zitacollapse. Tour guides,drivers,car rentals,food vendors and beach operators wote wataanza, au washaanza kuteseka na itaendelea kuwatafuna untill the top of food chain.

Chamsingi hapa njia ya fasta ya kunusuru utalii kama Serikali yaa mapinduzi ni kupromote utalii wa ndani pamoja na Kenya,Uganda,Sadc countries.

Punguzeni tozo kwa watalii kutoka Africa.. futeni bima sijui ya ajali kwa wananchi wote wa Africa na tangazeni Zanzibar iwe kama cheap destination kwa watalii wa Africa.

Zanzibari yetu nzuri inatakiwa ilindwe sana. Tuiokoe jamani focus kwa watalii kutoka South Africa,Botswana na Kenya. Warahisisheni kufanya utalii kuanzia kwenye boti mpaka visiwani hakika mtaokoa jahazi.

Nayaongea haya wakati nimelewa konyagi ya kati(500ml) niliyonunua kwa 12,000Tsh supermarket.. msinichukulie serious sana
 
Konyagi ya kati elfu 12000???
Maduka yote ya pombe ya mda mrefu hawana vibali vya kuagiza pombe. Sijui sababu ni nini. Ila kutaka utalii huku unawanyima watu vibali ku import pombe lazima usababishe pombe za ndani ziwe bei juu. Anyway naamini maamuzi yote wanayofanya serikali ya Mapinduzi na ya Busara na yamezingatia maslahi mapana ya Raia wao.
 
ni habari njema kwa mimi mtanganyika Zanzibar wakiwa na hali mbaya.
 
Konyagi ya kati elfu 12000???
Huyo amesema alinunua supermarket, but ni bei ya kawaida kwenye mabaa plus clubs.But sehemu za kishua lazima ipande na hii ni mahali popote duniani!!!!!!!
 
Imeshuka au sasa ni wakati wa Low Season?? Au wewe ni mgeni?? Tangu vita imeanza mwezi uliopita walikuwepo wa kutosha.
Post yangu nimetoa analysis. Sekta ya utalii ndio napopatia ugali wangu. Naijua nje ndani. High season iliyopita ni kama low season ya kawaida na low season hii ni kama hakuna kitu. Wenye akili kubwa wamenielewa,wewe kaa kutaka kubishana. Nimetoa solution hapo juu.
 
Huyo amesema alinunua supermarket, but ni bei ya kawaida kwenye mabaa plus clubs.But sehemu za kishua lazima ipande na hii ni mahali popote duniani!!!!!!!
Mzee hii post yangu ni analysis ya kitalii na uchumi. Maduka makubwa na importers wa pombe wakubwa hawana vibali. HAWANA VIBALII,IMPORTED SPIRITS,VODKA,RUMS AND WHISKEY HAWA IMPORT TENA. Hebu niambie sehemu gani au duka gani stonetown wanauza konyagi ndogo(200ml) chini ya 6k,ya kati chini ya 12k?
 
ni habari njema kwa mimi mtanganyika Zanzibar wakiwa na hali mbaya.
Zanzibar ni very important,Zanzibar ikipitia kipindi kigumu kaa ukijua Tanzania lazima i cover. Pesa yako ya madini na machungwa yako itatumika kupooza maisha magumu ya visiwani. Na hiyo ni Lazima hata Rais ungekua wewe. Inshort Zanzibar ni sehemu nyeti na Tanzania bara itailinda na kuisaidia kwa hali yoyote. Usije ukaichukulia poa kwa mihemko yako ya kisiasa lakini kwenye sekta ya ulinzi na usalama wa Tanzania Bara Zanzibar ni Muhimu kuliko mkoa wa kilimaanjaro na mlima wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…