BIG BROTHER ALEX
JF-Expert Member
- Sep 24, 2025
- 1,293
- 2,265
SEHEMU YA KWANZA 1
Habari zenu wakuu, mi ni kijana wa kawaida niko end of twenty something najianda kuingia thirty.
Katika pulukushani za maisha Dodoma na Arusha nilipata wazo la kujichanganya Zanzibar.Niliingia Zanzibar lengo ni utafutaji, sikuwa na pakufikia nilikuwa nanyoosha TU barabara mpaka tapo pata mahala pa kujihifadhi.
Nilizunguka sana mpaka usiku ukaingia, ya pata saa mbili, nikajisogeza msikitini kusali, baada ya hapo nikajipumzisha kidogo na uchovu, badae nikastuka naamshwa, vipi sheikh muda wa kufunga msikiti Usha fika, nikanyanyuka nikabeba mizigo yangu nakuondoka msikitini, nilianza kuzunguka nipate kivaranda Cha duka nijiegeshe, mpaka pakuche, nione itakuwaje kwa mapenzi ya mungu, watu walionyesha hofu sana juu yangu kunipokea ikizingatiwa ilikua usiku na mi ni mgeni ndo kwanza nimetoka bara.
Niliwakuta wanaume wawili wakiwa wamekaa wanapiga stori mbili tatu, niliwasalimu habari zenu tafadhali, waliniangalia kama wananisikilizaa shida yangu ni ipi, samahani ndugu zangu mi naitwa Ali nimetokea bara nimekuja Zanzibar kutafuta maisha ila kwa bahati mbaya Sina ndugu huku, nimefika asubuhi Kuna mwenyeji nilipata akahaidi kunisaidia pa kulala, lakini ilivo fika usiku kanibadilikia, na kunifukuza naombeni nipate, pakujiegesha asubuhi nianze kuangalia utaratibu mwingine.
Nikaona wanaangaliana kama wanatafakari kitu, jamaa wa kwanza:umesema umetokea wapi
Mimi: Arusha kaka
Jamaa wa kwanza: huku umekuja kufanya nini?
Mimi: kutafuta kazi. Abdallah: Sasa mbona unamizigo mingi sana, kawaida tunapo enda kutafuta kazi mahala Fulani ugenini Huwa tuna beba kibegi kidogo TU nguo tatu kwisha mambo mengine mbele ya safari bhana,
Nikaona wanajadili mambo Fulani badae dullah akanambia subiri hapo Kuna sehemu nataka nikupeleke, nikakuombee hifadhi.
Mimi nikakaa aisee bega si langu ni kweli nilibeba nguo nyingi sana vitabu vya chuo na nyaraka mbalimbali SIKUTAKA Hawa wajue hayo niliwahakikishia ni nguo TU. Nilikua hoi balaa uchovu wa safari, kumbuka Niki Toka Arusha na treni kuja dar, treni ni usafori mzuri sana kwa safari za kitalii nilienjoy sana, kwa kweli lakini sababu ya kupanda treni ni nauli nafuu kutoka Arusha kwa treni ni elfu kumi na name ilihali kwa basi ni arobaini Hadi hamsini. Hivo niliona Bora treni.
Muda kidogo dullah akaninyanyua tukaanza safari ya kwenda sehemu, sikupajua japo mi nilitegemea tunaenda ghetoni kwake na dullah au kwa Wana, lakini nikashangaa tunaenda sehemu kama soko hivi, kadri tulipo zidi kwenda ndo nikagundua kweli tumo sokoni, tukafika sehemu nikaona kama Kuna mtu kalala kwenye benchi, dullah akamwamusha oyi jamaa niambie bwana vipi lakini, yule jamaa akaamka, alikua amevaa koti, baadae ndo nilitambua kuwa ni mlinzi wa pale.
Dullah: Sasa sikia huyo dogo ni mbara kafika hapa Zanzibar kutafuta maisha lakini mwenyeji alimpata mchana kamgeukia huenda alikosa Imani nae akamfukuza hivo, naomba apate hifadhi hapa asubuhi, tutacheki utaratibu mwingine. Jamaa hakuwa na shida akakubali, ahh poa weka mizigo chini sogea pale kwenye benchi, ndo utalala hapo, kumbuka hiyo ndo siku yangu ya kwanza hapo Zanzibar, nikasogea kwenye benchi na kujipumzisha, huku namshukuru mungu.dullah aliondoka nahisi alienda kwake.
Asubuhi na mapema dullah kafika oyi vipi, mambo yanasemaje kaka, Mimi nikamjibu asee kwema nashukuru mungu sana japo, sikumwambia changamoto za usiku nilizo kutana nazo mbu zilikua zinapiga mpaka naamka kukaa, noma sana.
Sasa amka twende huku, tukaongozana na dullah kushuka maeneo ambayo kumbukumbu zangu ndo Yale niliyo pita Jana usiku kipindi natafuta hifadhi, Tulifika kwa mama mmoja muuza supu na boflo, dullah akaniagizia na yeye akachukua tukaanza kupata baaada ya hapo akalipa tukasepa, dullah akaanza kunihoji tulipo kua njiani.
Dullah: una fani Gani
Mimi: Sina fani yoyote labda mapishi ya vitafunwa kama maandazi half cake, chapati, vitumbua nk
Dullah: aha kumbe basi poa usijali, Sasa Kuna msukuma mwenzako hapo anauza matikiti hapa sokoni anatafuta mlinzi, vipi utaweza?
Mimi: Ndio taweza nimelinda sana Dodoma na Arusha hivo si mgeni wa hiyo kazi.
Dullah:aha kumbe, basi sawa ngoja tukamsikilize.
Tukaelekea pale kwa huyo ngosha, tulivo fika wakasalimiana na dullah, mi nipo pembeni nawacheki TU, wakazungumza badae ngosha akaniita pembeni, nikaenda.
Ngosha: mambo vipi
Mimi: kwema kaka nambie
Ngosha: hii kazi ya ulinzi wa matikiti utaweza kweli
Mimi: ndio taweza Nisha Fanya sana kazi ya ulinzi muda mrefu mno sioni ikinishinda.
Ngosha:basi poa mi takuwa nakulipa ef tatu kwa siku, hapo vipi
Mimi: sawa tu hakuna shida
Ngosha: basi poa jitahidi uwe una wahi saa kumi na mbili uwe hapa sawa, Mimi hakuna shida,
Tukaagana mi nikaondoka kumfata dullah, nilivo fika akaniuliza kama tumesha kubaliana, nikamjibu ndio Kila kitu tayari akaniuliza atakupa shingapi nikamjibu elfu tatu, akanambia basi poa hakuna shida, nika sema sawa, dullah akanirudisha pale ofisi ya furniture nilipoweka mizigo yangu tukakuta washa fika kazini wote mafundi na washikaji,
Kimbembe kikaanza baada ya kujua kinacho endelea wakaanza kumlalamikia Dulla, kwa nini anikaribishe ilihali anijui, je kama ni mwizi, Dulla akawa anajitetea lakini upinzani ulikua mkubwa sana, mpaka Kuna muda nilimuonea huruma sana, dullah aliendelea kunitetea kwamba mi ni mgeni na haki ya kusaidiwa ndicho alicho kifanya yeye kama binadamu lakini wale jamaa wakagoma, mi tayari nikawa Nisha jiongeza tayari kuwa inabidi nicheki ustarabu mwingine haraka sana.
Basi baada ya inshu kupoa niliondoka nikasema ngoja nikatembetembe mtaani, nikashika barabara sikujua hata naenda wapi, mi nikanyoosha tu, mungu mkubwa sana huwezi amini hiyo ilikuasiku yangu ya pili visiwani lakini sikupata shida kukariri njia nikasonga moja kwa moja nilitembea mpaka nikajikuta na fika stone town forodhani, nika kaa pale kujipumzisha kidogo nisubiri muda wa kazi niingie lindoni.
Ilipo timu saa kumi na moja hivi nikaanza kupanda ndogondogo huku nauliza pale ambapo nilitaka kupotea, kwa bahati nzuri nilifika sokoni nikapitiliza kwa ngosha, sababu mi mwenyewe nilikua nakaa hapo hapo sokoni, nikakbidhiwa nakuanza kazi rasmi, badae dullah naye alifika, tukalinda wote Hadi asubuhi huku akini sisitiza kuwa makini na wizi.
Maisha yaliendelea mpaka ikafikia hatua Dulla alikua hafiki hapo ofisini nahisi, alisha jiridhisha na tabia yangu na ustahilimivu kwenye kazi.
Niliendelea na kazi, Sasa bhana kwa sababu mizigo yangu ilikua pale kwa wajamaa wa furniture nilikua naenda kubadili na kuchukua vitu vichache, kuoga nilikua naogea msikitini nabadili nguo huko narudisha chafu naingia mtaa, baada ya kuona maneno yamekua mengi hapo ofisini kwenye furniture nikajaribu kufanya upelelezi kwenye vibanda vya mabati hapo sokoni, nikagundua Kuna kibanda kimoja kipo wazi ndani kipo vizuri tu japo mazingira ya nje si ya kutumia ia, nika ona potelea mbali, nikapasafisha nikaenda nikachukua mizigo yangu nikahamia humo kwenye hicho kibanda.
Nilikua humo, baadae wale jamaa wa furniture wakagundua, mana si mbali sana na ofisini kwao hapohapo soko la Banda maiti wakaanza tena maneno na kunifuatilia, nilivo ona hivo nikaanza harakati za kusaka chumba mana si nilikua nalipwa elfu tatu Kila siku pale sokoni, za ulinzi.
Siku hiyo asubuhi kwenye pitapita zangu, nikabahatika kuona chumba kimefungwa ni kama lilikua kibanda Cha biashara ila kinaonekana kama hakitumiki nikaulizia watu nikaambiwa nizunguke kule nyuma taona mlango hapo ndo wahusika walipo.
kweli, nilifika nikampata dada mmoja, nikaongea nae, akanambia hicho kibanda kinapangishwa, nikamwambia nakitaka nikamdanganya takitumia kutengeneza sabuni, yule dada akadai Sasa subiri niongee na mwenye nyumba takupa jibu chukua namba zangu, kweli nikachukua namba zake, tukawa tunawasiliana lakini akadai bado hajampata baba mwenye nyumba.
Zilipita siku huku napo kaa pale sokoni, wale jamaa wanaendelea kunifuatilia, siku hiyo nimepita pale kwa yule sista nika mkuta, akanambia mi nilipie tu nianze kupatumia atakuja kumpa mwenye nyumba pesa yake nikasema sawa tulikua tusha kubaliana takua nalipia ef 25kwa mwezi mana kibanda ni kidogo sana alafu kimo ndani sana ya mtaa, Yani ni uswaz lakini watu hamna sijui wanaendaga wapi.
Sikupoteza muda nikaanza kufanya usafi punde nilipo maliza kulipia, nikasafisha kweli kwani baada ya kufungua nikagundua hamna sakafu chini ni dongo tupu na mashimo ya panya makubwa, sikuogopa niliendelea na usafi nikamwaga maji, pakawa safi.
Sikupoteza muda nikaelekea KULE juu Banda Maiti kubeba vitu vyangu, nilihamisha kwa makundi kidogo kidogo mpaka nika maliza, nikawa nisha hama na kuanza maisha rasmi mjini unguja.
Itaendelea