YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
Zanzibar ndio imekuwa ikiamua Rais wa muungano awe nani
Mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana kuwa taifa moja la Tanzania. Swala likaja nani awe Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania? Nyerere hakutaka kujikweza akaona amwambie Rais Karume kuwa awe yeye Karume. Karume akakataa katakata akasema mimi bado sina uzoefu ndio nimetoka kufanya mapinduzi shika wewe Nyerere. Nyerere akashika Urais wa Zanzibar baada ya kupendekezwa na Mzanzibari Karume.
Mwaka 1984 Nyerere alitangaza nia yake ya kuwa ifikapo 1985 ataachia uraisi hatagombea tena uraisi atampisha mwingine.Wakati huo Raisi wa Zanzibar alikuwa Sheikh Aboud Jumbe na ndiye aliyetarajiwa kumrithi Nyerere kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1985
Lakini kundi la Wazanzibari likiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Seif Shariff Hamad liliibua hoja nzito kuwa Aboud JUMBE anataka kuvunja muungano ikabidi ajiuzulu uraisi hivyo pia Wazanzibari wakasababisha akakosa nafasi ya kuwa Raisi wa Muungano. Wazanzibari wakapendekeza Mzanzibari Ali Hassan Mwinyi ndie awe Rais wa muungano Nyerere akakubali na akawa Rais kweli 1985.
Rais Mwinyi Mzanzibari alitawala hadi mwaka 1995 akampendekeza Benjamin William Mkapa kuwa Raisi wa Muungano na kawa kweli raisi wa muungano.
Raisi Mkapa akatawala hadi mwaka 2005. Ilipofika 2005 ilionekana kuwa inatakiwa iwe zamu ya Wazanzibari na Mzanzibari aliyekuwa na nguvu kubwa NA SIFA NYINGI alikuwa Salim AHMED salim. Lakini Wazanzibari wakamkataa kumpa kura kisa eti alikuwa chama cha HIZBU na ndie alihusika mpango wa kumuua Karume.
Kwahiyo kura kwenye chama wakampa Jakaya Mrisho KIKWETE wakampiga chini Mzanzibari mwenzao na kumpa Kikwete.
Kikwete akatawala hadi 2015 IKatakiwa naye akabidhi uraisi kwa mwingine.Wakajitokeza Wazanzibari mmojawapo ambaye alikuwa na sifa lukuki ni mwanamama Amina Salum Ali ambaye aligombea kuchaguliwa na CCM na angeweza kupita lakini akatibua.Kulikuwa na kundi moja kubwa sana ndani ya CCM linaitwa mtandao lilikuwa chini ya Lowasa na lingine lilikuwa chini ya Bernard MEMBE
Haya makundi hasimu yaligawana wajumbe na kukigawa chama.CCM Wakaona isiwe kesi wakaona kundi kubwa liko nyuma ya Lowasa na CCM ikawa haitaki makundi wakakata jina la LOWASA asiendelee kuwa mgombea .Majina yakabaki ya wagombea wengine akiwemo AMINA SALUM ALI
Sasa kwenye kujieleza AMINA SALUM ALI akachemka akasema yukop pamoja na kundi la Lowasa ili akivizia kupata kura za kundi la wajumbe wa Lowasa wakati hawakuwa naye pamoja toka mwanzo!!! Akpigwa chini na Membe naye akapigigwa chini kuwa ni chaguo la Kikwete eti mdogo wake wa kuzaliwa!
Mwisho wa siku sababu ya AMINA SALUM ALI kujichanganya akatoa nafasi kwa Magufuli kuwa Raisi wa MUUNGANO badala ya yeye sababu asingejionyesha kuwa na kundi wangekutana na Magufuli na uwezekano mkubwa angeshinda.Hivyo mzanzibari tena akasaidia kuamua nani awe Rais wa muungano.
Ikafika kuchagua makamu wa Rais awe nani na lazima atoke Zanzibar.Na ilikuwaa imeamliwa kuwa Mgombea uraisi akiwa mwanaume mgombea mwenza awe mwanamke na mgombea uraisi akiwa Mwanaume mgombea mwenza awe mwanaume.
Sasa tena ile na nafasi ya mgombea mwenza alitakiwa apewe AMINA SALUM ALI lakini sababu alijionyesha kuwa na makundi wakamshtukiza na kumpa Mama SAMIA SULUHU Hassan.
Wazanzibari kwa mara ingine wakaamua nani awe nani.
Magufuli aliongoza hadi 2020 ilipofika uchaguzi inasemekana Raisi Magufuli alimtaka Hussein Mwinyi ndie awe mgombea wake mwenza na Profesa Mbarawa ndie awe Raisi wa Zanzibar.Wazanzibari wakakataa wakasema anataka kumuweka Mbarawa Zanzibar ili aiburuze zanzibar ndio maana anataka Hussen Mwinyi awe mgombea mwenza. Wanzazibari wakamnyima kura Mbarawa wakampa Mwinyi kura za maoni, wakampa Magufuli, SAmia ndie aendelee naye kama mgombea mwenza.Magufuli ikabidi aendelee na Samia Suluhu kama makamu wa Rais.
Katiba inasema Raisi akifariki Makamu ndiye anayeshika. Kafariki Magufuli, Mama SAMIA ndie kashika. Hiyo nafasi ilikuwa ya Hussein Mwinyi kama anngekuwa alikubali kuwa mgombea mwenza. Lakini wazanzibari wakamkwepesha. Ndio maana Mama Samia ana haki ya kusema Mwenyezi Mungu ndio kamuwezesha kufika alipo.
Mchango wa Zanzibar ni mkubwa kwenye muungano.