GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Namba hazidanganyi!
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2022, Zanzibar ina ukubwa wa kilomita za mraba 2,460 na watu 1,889,773. Imeuzidi mkoa mmoja tu wa Tanganyika, Dar Es Salaam!
Dar Es Salaam ina ukubwa wa kilomita za mraba 1,393. Hata hivyo, inaizidi Zanzibar kwa idadi ya watu. Kwa mwaka 2022, Dar Es Salaam ilikuwa na watu 5,383,728.
Pamoja na Zanzibar kuwa ndogo kieneo na kiidadi ya watu, imejithibitisha kuwa si ndogo kiakili! Imeweza kuitawala nchi kubwa iitwayo Tanganyika.
Wanaofikiri Zanzibar ni koloni la Tanganyika wanajidanfanya! Ukweli ni kwamba Tanganyika ndiyo koloni la Zanzibar.
Nimeisikiliza clip ya mwanasiasa mmoja akiilinganisha Zanzibar na Tanga. Kwamba, pamoja na kwamba Tanga ni kubwa kuliko Zanzibar, ina wabunge 12 tu huku Zanzibar ikiwa na wabunge 80. Mkoa wa Tanga una kilomita za mraba 26,677 na watu 2,615,597(kwa mwaka 2022).
Kwa kuwa Mzanzibar anaweza kuitawala Tanganyika lakini Mtanganyika akiwa Zanzibar ni mgeni, na kwa kuwa Mzanzibar ana haki ya kujisikia yupo nyumbani akiwa Zanzibar na Tanganyika tofauti na Mtanganyika ambaye Tanganyika pekee ndiyo kwao, na kwa kuwa Zanzibar inajitawala na kuitawala Tanganyika, ni dhahiri shayiri kuwa imeizidi Tanganyika kiakili. Ni ndogo kieneo lakini ni kubwa kiakili!
Acheni Wazanzibar wapewe maua yao!