Zanzibar: Rais Mwinyi afanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais Hussein Mwinyi amemteua Mshenga Haidar kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO). Vilevile amemteua Nassor Ameir kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF).

Shariff Ali anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji (ZIPA) huku Suleiman Hamis akiteuliwa na Dkt. Mwinyi kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Utangazaji.

Aidha, Dkt. Huda Yussuf ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) na Hartha Ali anakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe.

Pia, Rais amemteua Abdulla Mzee kuwa Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…