Katika Hali ya kushangaza Chama Cha ACT Wazalendo kupitia Makamo wa Rais Zanzibar kimefichua kupata mwaliko wa kuonana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri Samia Suluhu Hassan.Hayo yamefanyika huku Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alibambikwa kesi ya Ugaidi na wakuu wa Serikali wakionekana wazi wazi kuingilia mhimili wa Mahakama kuhusu kesi hiyo.
Ifuatayo ni habari iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi Kama alivyonukuliwa Makamo wa Rais Zanzibar Othman Massoud.....
Rais akutana na ACT na kufikia muafaka huku akipiga danadana kuonana na CHADEMA
Makamo wa Rais Othman Massoud afichua Siri hiyo
Alisema walipata wito wa Rais Samia wa kuonana naye Unguja na alikwenda yeye, makamu mwenyekiti wa chama hicho, Zanzibar Juma Duni Haji na Naibu Katibu (Zanzibar), Nassor Ahmed Mazrui.
Wengine ni Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho, Salim Biman na mwanasheria wa ACT-Wazalendo Omar Said Shaaban.
“Tukamueleza kuwa hatukukwama labda hatukueleweka. Tukamwambia njia na hoja zetu ni hizi kama tulivyoeleza Pemba hatuna cha kubadilisha.
“Tulifikia mwafaka kuwa watakwenda kukaa na kuchukua hatua, hatua ndiyo hii mliyoiona, operesheni imefanywa tumesema tulieleze hili pengine hakukuwa na haja ya kulizungumza. Lakini tunasema ili dunia itusikie,kama ni changamoto za kifamilia sawa,” alisema Othman.
Maoni ya Wananchi baada ya Rais kukutana na ACT kisiri Unguja
Ni vyema Ikulu ikaweka hadharani mazungumzo haya na kilichoamuliwa kwani Kama si Makamo wa Rais Zanzibar kufichua Siri isingejulikana.
Pili wananchi hasa upande wa bara wanaweza kuhisi upendeleo fulani wa kieneo kwa sababu kwanini Rais aende kisiri kukutana na ACT huko Unguja na kutatua mtanziko wa kisiasa lakini kwa upande wa Bara kiongozi wa Chama kikuu anafunguliwa mashtaka ya kubambika ya Ugaidi.
Kuna mambo mengi ya kujiuliza lakini Ni vyema Ikulu wakaondoa hofu hii mapema