TRA Tanzania
Senior Member
- Jul 16, 2022
- 128
- 370
Naibu Kamishna Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA - Zanzibar Bw. Saleh Haji Pandu amesema wataendelea kuvilea vilabu vya kodi mashuleni ili kuwaandaa watoto kuwa walipokodi wazuri wa baadae na kuwa mabalozi kwa jamiii juu ya ulipaji kodi kwa hiyari.
Bw. Pandu ameyasema hayo tarehe 23/11/2024 kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano ya vilabu vya kodi kwa shule za sekondari za Unguja Zanzibar ambapo Skuli ya Sekondari ya Haillesellasie imeshinda nafasi ya kwanza katika uwasilishaji wa mada , Skuli ya sekondari ya Biashara imeshinda nafasi ya kwanza katika Maswali ya papo kwa papo, Skuli ya Zanzibar Feza imeshinda nafasi ya kwanza katika ukusanyaji wa risiti za kielecroniki na skuli ya Trifonia Academy imeshinda nafasi ya kwanza katika uandishi wa Insha.
Washindi hao walitunukiwa zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Desktop Comouter, Jezi za mpira, tuzo, rimu za karatasi, mabegi pamoja na chupa zenye nembo ya TRA.