Zanzibar Tunasubiri sehemu yetu ya Fedha za (BAE UK) kwa TZ

Sonara

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2008
Posts
726
Reaction score
70
Inatubidi tuwe tunakumbushana mapema ili kuepusha mivutano .
 
vultures.

Watu wa aina hii ndiyo wale wale wanaotoa macho wazazi wao wafe ili wapate urithi, wakiji convince ni "hela zetu".

Unaweza kuweka figures za contribution ya Zanzibar katika our meager GDP?

Ingefaa kuangalia haya mambo.

"God" bless the child that has got his own.
 
Inatubidi tuwe tunakumbushana mapema ili kuepusha mivutano .
Kwenye migawo mna super memory eeh!
Mbona kwenye kununua mlikuwa pua chini, na wakati tunalalama juu ya ufisadi wa hii maneno mlikuwa kando mnapiga gahawa!!
 
Hahahaha umeme tu mmesahaulika hizo pesa tayari zimesha undiwa kamati ni za uchaguzi kwa ajili ya kuwaghalagaza.
 
kutoka TZ au Tanganyika??? mbona unaconfyuzi mambo? au hata historia hujui.jibu pls...
"SALUTE"
 
acheni kufanya kazi, kwa mategemeo ya kupata vya bure tu, Watu wengine taabu kwelikweli,samaki mbona mlisusia???
 
Inatubidi tuwe tunakumbushana mapema ili kuepusha mivutano .
acha uchokozi yakhe, kwenye fweza unasema tunasubiri fweza yetu kama Watanzania ila kwenye mafuta kwenye kikombe ya Wazanzibar tu na sio Watanganyika! hatuna hiyana 4.5% ya hizo watakazotoa BAE ni halali yako!
 
acheni kufanya kazi, kwa mategemeo ya kupata vya bure tu, Watu wengine taabu kwelikweli,samaki mbona mlisusia???

Kwa tarifa yako samaki hawakususiwa, isipokuwa moja kati ya miongoni mwa sifa za wazanzibari ni kinai na kutokana na kinai hiyo ndio wakasema madhali kutokea mwanzo hamkuwa na niya ya kugawa kama katiba ninavyosema na kujifanya hamnazo , ndipo hapo wazanzibari wakasema kuleni nyie hao samaki,lakini basi pia ifahamike unapokuwa na mshirika anapenda kufakamia hata cha mwenziwe katika mazingira yeyote yale mtu kama hao anakuwa na sifa ya shida kuzivalia kibwebwe.
 

He! nilikua sijui hivi kumbe na samaki wa magufuli wa mwaka jana ni moja ya mambo yaliyopo kwenye muungano?....
 
...kinai.......duh!mambo ya kiswahili bwana..!sasa kwa nini na hizi wasizikinai...?!au sababu hazina uvundo wa samaki (just kidding....)
 
mkiwakataa samaki wenzenu walioko bara huku watakula.😀😀:
 
Inatubidi tuwe tunakumbushana mapema ili kuepusha mivutano .

Hizo hela zinaenda kwenye Serikali ya Muungano wa Tanzania meaning Zanzibar included. Wakati rada hiyo ina nunuliwa pesa zilitoka kwenye serikali ya muungano siyo kwamba Zanzibar iliombwa itoe pande ya bajeti yake kwa ajili ya rada. SO usijali mkuu cha muungano ni chenu pia. Hizo pesa zita wanufaisha pia.
 
Ni bora mkaanza kwanza na kukagua vitabu vya People's Bank of Zanzibar (PBZ) toka enzi hizo. Halafu wanahisa wake mnawafahamu?
 
Hizi pesa hazitarudishiwa serikali kwani wao walipata mgao wao yaani kupata rada. Kwa taarifa tu pesa hizi zitapelekwa kwenye vyama vya kijamii (charities) au bongo tuna NGOs kibao. Kama zanzibar mnaweza anzisheni NGOs nyingi ili mpate mgao

 
Inatubidi tuwe tunakumbushana mapema ili kuepusha mivutano .

Kwa kuwa mafuta bado ni suala la Muungano, chimbeni hayo mafuta huko Zenj na kuyauza ili mpate 4.5% yenu!
 
Hahahaha umeme tu mmesahaulika hizo pesa tayari zimesha undiwa kamati ni za uchaguzi kwa ajili ya kuwaghalagaza.

Naam hizi zote zitaingia katika mfuko wa hazina ya CCM kwa ajili ya October 2010.
 
Kama nimeelewa vyeama ni kwamba hizo $28M ni kiasi kilichozidi baada ya bei kuzidishwa, hivyo basi pesa hizi zitarudi kule zilikokuwa. Hili sio pato ni pesa zilizozidishwa makusudi na wajanja ili wajipatie vijisenti. Hivyo zitarudi zilikotoka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…