Zanzibar Tunasubiri sehemu yetu ya Fedha za (BAE UK) kwa TZ

Zanzibar Tunasubiri sehemu yetu ya Fedha za (BAE UK) kwa TZ

YAKHE nakuunga mkono. Lakini pia wale wachapishaji na wahariri wa Business Times Limiited ambao mwaka ule walitoa stori kwenye gazeti lao la Majira Jumapili (ingawa baadhi marehemu sasa) inafaa pia walipwe kitu kutokana na mchango wao wa kuwafungua macho wa Tanzania kuhusu dili ya Rada bomu.Vilevile ikumbukwe jamaa hawa walisumbuliwa sana na DG wa wakati huo pale makao makuu ya Wizara ya ndani na kuadhibiwa kwa kusimama muda mrefu bila sababu na kisha kutiwa lokapu.Ni haki yenu na ni haki ya wachapishaji na wahariri wa BUSINESS TIMES LIMITED wakati ule pia kulipwa fidia kutokana na usumbufu wote huu na kuwachafulia jina lao kwa kuwaita eti ni wachochezi na Watanzania wasioipenda nchi yao. Jamani hii ni haki yao wapeni!!!
 
WALIPENI pia Wchapishaji na Wahariri wa Business Times waliotiwa ndani mwaka 1994 kwa kisingizio cha uchochezi wakati walikuwa wakifichua mchezo mbaya kwenye dili hiyo ya rada!
 
Kama nimeelewa vyeama ni kwamba hizo $28M ni kiasi kilichozidi baada ya bei kuzidishwa, hivyo basi pesa hizi zitarudi kule zilikokuwa. Hili sio pato ni pesa zilizozidishwa makusudi na wajanja ili wajipatie vijisenti. Hivyo zitarudi zilikotoka!

Sure, hizi fedha zikianza kupelekwa sehemu ambako hazikutoea itakuwa ni misallocation of resources na itabidi tena tuanze kufuatilia!
 
Back
Top Bottom