YAKHE nakuunga mkono. Lakini pia wale wachapishaji na wahariri wa Business Times Limiited ambao mwaka ule walitoa stori kwenye gazeti lao la Majira Jumapili (ingawa baadhi marehemu sasa) inafaa pia walipwe kitu kutokana na mchango wao wa kuwafungua macho wa Tanzania kuhusu dili ya Rada bomu.Vilevile ikumbukwe jamaa hawa walisumbuliwa sana na DG wa wakati huo pale makao makuu ya Wizara ya ndani na kuadhibiwa kwa kusimama muda mrefu bila sababu na kisha kutiwa lokapu.Ni haki yenu na ni haki ya wachapishaji na wahariri wa BUSINESS TIMES LIMITED wakati ule pia kulipwa fidia kutokana na usumbufu wote huu na kuwachafulia jina lao kwa kuwaita eti ni wachochezi na Watanzania wasioipenda nchi yao. Jamani hii ni haki yao wapeni!!!