Zanzibar 2020 Zanzibar: Vikosi vya Usalama vyapiga mabomu ya machozi, wananchi wakimbia na kuacha mitaa ikiwa mitupu. Huduma za kijamii zasimama

Stone Town

Senior Member
Joined
May 28, 2007
Posts
114
Reaction score
26
Askari zaidi ya 20, wakiwa ndani ya magari yao asubuhi ya leo wanafyatua mabomu ya machozi kwa kila kundi la watu wanalokutana nalo.

Katika eneo la Darajani, askari hao bila kuwepo kwa viashiria vya uvunnjifu wa amani, wamefyatua mabomu ya machozi kwa kundi dogo la watu waliokuwa pembezoni mwa Barabara za Mkunazini.

Hali hiyo imezua taharuki huku watu wakikimbia kuokoa maisha yao.

Katika eneo la Soko Kuu la Zanzibar, Marikiti, sehemu kubwa ya soko hili imefungwa na hakuna wafanyabiashara, isipokuwa wazee wachache wanaopanga nyanya, bamia na matango machache pembezoni mwa soko hilo.

Nimeshugudua maduka karibu yote yamefungwa tangu asubuhi na hakuna mizunguko ya watu, kama ilivyozoeleka katika eneo la Darajani na jirani.



Taarifa zaidi zinafuata...
 
Mnawaua halafu mtamtawala nani nyie vichaa? au mtayatawala mawe?!

CCM huu uhuni mnaowafanyia raia wa nchi yetu kwasababu ya uroho wenu wa madaraka sasa mnakoelekea siko.

Najiskia naanza kupoteza heshima kwa Mzee Mwinyi niliyekuwa nikimheshimu sana.

Picha zinaonesha majengo yamechoka, mji umepauka, lakini bado mashetani yanalazimisha kuendelea kuwatawala tu, waacheni wamuweke kiongozi wanayemtaka awaletee maendeleo ya kweli.
 
Makaburu wa afrika ya kusini nao walikuwa hivihivi,akili zilipowajia wakatambua kuwa wanachokifanya siyo sahihi, akajitokeza kaburu miongoni mwa makaburu haohao akafanya jambo la haki kwa kukaa meza moja na watu weusi,huo ndio ukawa mwisho wa mateso ya wananchi wa afrika ya kusini na amani ikatawala mpaka leo.

CCM wasifikri kuwa watakaa milele na milele madarakani, pamoja na kufurahia manyanyaso pamoja na mauaji kwa raia wanao dai haki inayoporwa na CCM, wakumbuke kuwa ipo siku wataondoka madaraka kwa nguvu ya umma hiihii au miongoni mwa wanaccm wenyewe atatokea mtu ambaye nuru itamwangazia na kutambua kuwa kitu wanachowafanyia wananchi siyo sahihi na kuamua kutenda haki,kama kaburu wa afrika ya kusini na amani itatawala tanzania.
 


Mimi nshapotezea heshima toka ile siku alisema Magufuli atawale miaka 15, alikuwa analinda ugali wa kizazi chake.
 
Ukiona wanazingua usikubali kamanda chukua mawe kawapige ffu Kaka amstedamu atakutetea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…