Stone Town
Senior Member
- May 28, 2007
- 114
- 26
Askari zaidi ya 20, wakiwa ndani ya magari yao asubuhi ya leo wanafyatua mabomu ya machozi kwa kila kundi la watu wanalokutana nalo.
Katika eneo la Darajani, askari hao bila kuwepo kwa viashiria vya uvunnjifu wa amani, wamefyatua mabomu ya machozi kwa kundi dogo la watu waliokuwa pembezoni mwa Barabara za Mkunazini.
Hali hiyo imezua taharuki huku watu wakikimbia kuokoa maisha yao.
Katika eneo la Soko Kuu la Zanzibar, Marikiti, sehemu kubwa ya soko hili imefungwa na hakuna wafanyabiashara, isipokuwa wazee wachache wanaopanga nyanya, bamia na matango machache pembezoni mwa soko hilo.
Nimeshugudua maduka karibu yote yamefungwa tangu asubuhi na hakuna mizunguko ya watu, kama ilivyozoeleka katika eneo la Darajani na jirani.
Taarifa zaidi zinafuata...