Zanzibar 2020 Zanzibar: Vikosi vya Usalama vyapiga mabomu ya machozi, wananchi wakimbia na kuacha mitaa ikiwa mitupu. Huduma za kijamii zasimama

Hauwezi mtu ukawatangazia wafuasi wako wafanye fujo then polisi wabaki wanakuchekeeni hii haiwezekani.
 
Reactions: mmh
Masikini!!! Jeshi limekuwa nyenzo ya kisiasa ya kuwashambulia wananchi!

Pole Tanzania!
 
ulafi wa madaraka
 
Mnaleta utani kwenye roho za watanzania, nyie ni laana ya hili taifa.

Naendelea kutazama picha za vijana waliouawa jana usiku na vikosi vya usalama, hali ni ya huzuni sana kwa wapemba.
so sadness
 
kama hatuta kuwa hai bhasi tutakuwa tumekufa ila zanzibar itakuja kuwa nchii yakujitegemea alafu itakuwa tajiri sana
 
Una uhakika Afrika Kusini amani inatawala hadi leo?
Kama amani haipo tatizo halitokani na unyanyasaji wa makaburu tena, tatizo litakuwa linafanana na la kwetu linalosababishwa na watawala waliopo madarakani.
 
..kama wako mita 200 basi wasibugudhiwe au kupigwa mabomu.

..sijui kwanini watawala wanakerwa na maneno "kulinda kura."

Utaratibu ndio ustaarabu na inabidi uheshimiwe, unafikiri watu wakiruhusiwa kulinda kura vituoni kutakuaje

Vitu vya kila mtu kufanya anachokitaka vinaweza kufanyika au kukubalika sehemu yenye utawala holela tuu na sio kwenye serikali thabiti
 
Hivi vikosi vya usalama vya Tanzania ovyo kweli, yaan yanapita yanapiga mabomu ovyo ovyo tu hata sehemu ambazo hakuna dalili zozote za uvunjifu wa amani, nendeni mtwara huko ambapo watz wenzetu wanateseka na waaasi wa Msumbiji kama kweli mna ubavu, askari wengine ni ndugu, majiran na rafiki zetu tunawajua vilivyo nje ndani msifikir hatuna uwezo wa kukabiriana na nyiny bali tunawaheshimu tu, wengi ni wepes mno hasa mkiwa hamna hizo silaha zenu.
 
..sijui kwanini watawala wanakerwa na maneno "kulinda kura."
Watapigwa na kutawanywa. Sirro kasema hawezi kuruhusu kila mwanachama wa chama cha siasa akakaa nje eti kulinda kura. Huo ni mwanzo wa vurugu.

Kama mawakala ndani watafanya wapaswayo kufanya, kura zinaweza “kulindwa” kwa Mkurugenzi siku ya kutangazwa kwa sababu by then Mbunge anaweza kuwa keshapata majumuisho ya kura kutoka vituoni.

Kama Mawakala kule ndani wakikengeuka, huko nje walindao kura wanapoteza muda tu
 

..mimi nadhani Sirro anashughulika na matokeo badala ya chanzo cha tatizo.

..Sirro alitakiwa awabane wahusika ktk tume za uchaguzi washughulikie malalamiko ya vyama mbalimbali ili kuepusha vurugu za wananchi.

..kwenye nchi za wenzetu integrity ya zoezi la kuandikisha wapiga kura, na kupiga kura, inalindwa kwa nguvu zote. wako tayari kuchezea mambo yote isipokuwa zoezi la uchaguzi.

..hiki anachofanya IGP Sirro kilishafanywa na ma-IGP waliopita kama Harun Mahundi, Omar Mahita, Saidi Mwema, na Ernest Mangu. Leo hii bado IGP Sirro anashughulikia tatizo lilelile kwa namna ileile ambayo watangulizi wake walishughulika nalo.

..Kwenye nchi za wenzetu huwezi kuona maaskari na mitutu, na magari ya deraya na washawasha, siku ya kupiga kura. The fact kwamba tunayashuhudia hayo hapa Tanzania ni ishara kwamba uchaguzi wetu una matatizo.
 
The fact kwamba tunayashuhudia hayo hapa Tanzania ni ishara kwamba uchaguzi wetu una matatizo.

This is it. As long as muundo wa NEC/ZEC unabaki ulivyo na fact kwamba matokeo ya Rais hayapingwi kokote, CCM hawatatoka madarakani

Ukiruhusu matokeo yapingwe then ni rahisi watu kugather evidence na kuzisubmit. Kwa sasa NEC wanaweza tu kubadilisha namba za kura za mtu na kumtangaza fasta na life likasonga tu as if nothing happened
 
Kama amani haipo tatizo halitokani na unyanyasaji wa makaburu tena, tatizo litakuwa linafanana na la kwetu linalosababishwa na watawala waliopo madarakani.
Usipende kuropoka vitu usivyovijua. Kukaa kimya wakati mwingine ni busara zaidi kuliko kujifanya mjuaji.
 
Uliza ilifanikiwaje uchaguzi wa mwaka 2010 Nyamagana??? 2015 Mbeya mjini, Kilombero, Tunduma, Momba, Arusha Mjini na Kawe????

Au Wewe ni mgeni kwenye kufuatilia chaguzi za Tanzania??
Endapo wakala tu aliyepo ndani hawezi “kulinda kura”, mtu anayesimama nje 100 meters uliambiwa mapema kwamba hana ubavu wa kulinda chochote especially pale ambapo Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni mwana CCM/DED/Mteule wa Magufuli anapoagizwa kufanya yake

Hii mbinu ya “kulinda kura” ilishafail kitambo. Hata hao uliowataja ni rare cases tu ambapo kwanza mawakala wao walisimama imara kuanzia kwenye kila kituo, wabunge wateule wakawa wameweka mtandao wao kukusanya na kujumuisha matokeo yote kutoka vituoni then wakaenda kumalizia tu kwa DED
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…