ZANZIBAR vs SOMALIA

ZANZIBAR vs SOMALIA

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
hadi sasa hivi mpira bado unaendelea. zanzibar 2 - somalia 0. over
 
somalia wanaonyesha hawana mazoezi lakini wana mipango mizuri ya kuche. zanzibar hiki kipindi cha pili fowadi wa zanz wakipata mpira wanalenga goli moja kwa moja.
 
dak ya 28 mpira unagonga mwamba wa somalia.
 
huyu fowadi wa zanz hamadi wamempasia mpira yeye na kipa alichofanya akaurudisha ulipotoka kama anaokoa vile. sijaelewa alikuwa na maana gani.suleiman kasi ametolewa nje
 
naona somalia wameamua. wanapigiana pasi si mchezo. wachezaji wa zanzibar washachoka. wametuumizia kanavaro wetu
 
agrey morris anafungia zanzibar goli la tatu kwa mpira wa kona aliopiga kichwa ukaingia moja kwa moja goli.mohamad mohamed kafunga goli la nne limekataliwa kwa sababu alikuwa kaotea.
zanzibar 3 - somalia 0
 
mpira umekwisha. Kama mchezo unaofuata Uganda wakiwafunga Burundi basi zanzibar itapata nafasi ya kusonga mbele.
ZANZIBAR 3 - SOMALIA 0.
OVER
 
kumbe na wasomali wamo mara hii!!! tuwakaribishe EAC tu
 
Back
Top Bottom