Zanzibar: Wamiliki wa Hotel kuchukuliwa hatua ikiwa wageni wao watatoka bila kuvaa stara

Zanzibar: Wamiliki wa Hotel kuchukuliwa hatua ikiwa wageni wao watatoka bila kuvaa stara

Safi sana. Utalii ni habari nyingine na mavazi ni habari nyingine, watalii wanapaswa kuheshimu mila, tamaduni na desturi za maeneo wanayotalii. Ndio maana nchi za wenzetu wanalinda sana taratibu, desturi na mila zao na bado utalii uko pale pale.
Ma hii ndio maana ya utalii haswaa yani unakuwa unavaa tamaduni za watu fulani kwa muda.

Acha wazungu wavae kama wazanzibari
 
Serikali ya Zanzibar imesema itawachukulia hatua wamiliki wa hoteli ambao wageni wao watatoka hotelini wakiwa hawajavaa nguo za stara. Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale amewataka wageni hasa watalii kutovaa nguo zinazokiuka maadili wawapo maeneo ya umma, mfano sokoni.

Chanzo: Swahili Times

Halafu baadae utasikia anasema anahamasisha utalii Zanzibar.
 
Ma hii ndio maana ya utalii haswaa yani unakuwa unavaa tamaduni za watu fulani kwa muda.

Acha wazungu wavae kama wazanzibari
Tena wanapendeza Mashallah!. Utalii sio kutembea uchi. Hata Saudi Arabia, Dubai utalii upo lakini hawatembei uchi.

Ombi kwa SMZ, watoe vipaumbele kwa wafanyabiashara wafungue maduka ya kuuza mavazi ya kujistiri maeneo ya Bandarini na Airport ili watalii wakifika bandarini na Airport waweze kununua khanga, madera na vitenge ili kujistiri.
 
Rafiki zangu walifanya kazi Arabuni nako walitakiwa kufanya hivyo. Kwenye compound mnayoishi unatembea unavyotaka lakini kwenda mjini na madukani ni lazima ufunike kichwa mwanamke na nguo istiri maungo. Wanaume pia huwezi kutembea tumbo wazi.

Hao unaowazungumza kwao utalii sio nguzo kuu ya uchumi, Itizame Dubai ambayo Utalii ni katika focus yao ilivyo, Na Kwa Zanzibar wao ni moja ya nguzo kuu kwahiyo wanachemka wanapojaribu kufany akama hivo. Wao wanawahitaji Zaidi hao watalii kuliko watalii wanavyowahitaji wao.
 
Kuhamasisha utalii sio kuacha watu watembee uchi.
Hakuna mtalii anatembea uchi.. kama yupo tuambie... wale wana taratibu zao na hela zao, nyinyi mnataka hela zao, ni lazima mnyenyekee
 
Safi sana. Utalii ni habari nyingine na mavazi ni habari nyingine, watalii wanapaswa kuheshimu mila, tamaduni na desturi za maeneo wanayotalii. Ndio maana nchi za wenzetu wanalinda sana taratibu, desturi na mila zao na bado utalii uko pale pale.

Hapana mkuu, hapo wamekwanga. Unapamua ku focus na utalii lazima ukubali kupeteza mambo mengine, Mfano mzuri ni Dubai. Sisi tunawahitaji wazungu sio wao wanatuhitaji sisi, kwahiyo sheria kama hizo hazitusaidii Zaidi ya kuwakimbiza hao watalii.
 
Tena wanapendeza Mashallah!. Utalii sio kutembea uchi. Hata Saudi Arabia, Dubai utalii upo lakini hawatembei uchi.
Ombi kwa SMZ, watoe vipaumbele kwa wafanyabiashara wafungue maduka ya kuuza mavazi ya kujistiri maeneo ya Bandarini na Airport ili watalii wakifika bandarini na Airport waweze kununua khanga, madera na vitenge ili kujistiri.
Dubai wanatembea uchi mkuu, au uchi unakusudia uwe kama mnyama? na huko Saudia wamelielewa hilo ndio mana wameanza kufungua ma night club na matamasha ya muziki ili kukuza utalii
 
Huyo waziri nae boya tu, utamlazimisha mtu avae ambavo hajazowea? Mtu kazoea kuvaa vipensi wewe utake avae madera inaingia akilini kweli hiyo?
Unakusudiwa kama hivi. Mbona Zanzibar watu wanavaa vipensi hata vimini n.k. Hakuna anaelazimishwa kuvaa dela wala baibui

But kama hivi ni too much...
20210302_165644.jpg
 
Huyo waziri nae boya tu, utamlazimisha mtu avae ambavo hajazowea? Mtu kazoea kuvaa vipensi wewe utake avae madera inaingia akilini kweli hiyo?
Hizo nguo za stara watakuwa nazo?
 
Safi sana. Utalii ni habari nyingine na mavazi ni habari nyingine, watalii wanapaswa kuheshimu mila, tamaduni na desturi za maeneo wanayotalii. Ndio maana nchi za wenzetu wanalinda sana taratibu, desturi na mila zao na bado utalii uko pale pale.
Ngoja waondoke mtawatafuta kwa tochi, hafu mtawaambia waje waishi kwa uhuru wanaoutaka
 
Serikali ya Zanzibar imesema itawachukulia hatua wamiliki wa hoteli ambao wageni wao watatoka hotelini wakiwa hawajavaa nguo za stara. Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale amewataka wageni hasa watalii kutovaa nguo zinazokiuka maadili wawapo maeneo ya umma, mfano sokoni.​

Chanzo: Swahili Times
kweli mambo ya Kale..

By the way angecheki kale mabibi na mababu zetu walivaa nini asingeongea hayo..., hizo ushungi n.k. zilikuja na mashua.
 
Back
Top Bottom