Zanzibar wanaliliaje hela ya FIFA na wao si mwanachama

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Nimeshangaa kuona ZFF wanalilia kugawana hela waliyopewa TFF na FIFA na wakati wao siyo mwanachama wa FIFA,pia wanajua michezo siyo jambo la Muungano.Zanzibar wanatakiwa watafute uanachama wa FIFA au michezo iwe jambo la Muungano.
 
Zanzibar kamwe haiwezi kupewa unachama kwa kuwa kwa vigezo vya FIFA, sio nchi bali ni sehemu ya Tanzania. FIFA inatambua members wa UN. Kuna exception ya United Kingdom kwa sababu za kihistoria. Hawataki tena kurudia kosa hilo.

Mgao wa hela ya FIAFA na mambo mengine inaweza kuwa ni local arrangement ndani ya TFF. Zanzibar iwe treated kama special zone na mgawo wao uwepo kikanuni.

Vinginevyo tutapiga sana kelele hadi kiama. Alipata uanachama wa CAf ukaja kufutwa na Rais wa sasa. Hiyo ingekuwa nhgao ya kuombea uanachama wa FIFA japo bado ingekuwa vigumu sana.
 
Kwani maana ya T.F.F ni nini?

"Not everything is for everybody"
 
TFF - Tanzania Football Federation

Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar.

Tuwagawie au tuwakatae tu? 😂
 
Ishu ya Zanzibar ni ngumu sana ,ipo ndani ya Tanzania halafu ina ligi yake tofauti,heri hata ligi kuu kungekuwa na vilabu toka Zanzibar halafu ZFF ifutwe
TFF - Tanzania Football Federation

Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar.

Tuwagawie au tuwakatae tu? [emoji23]
 
Kinachotuuma sisi wazanzibar ni kupata mgao kama mkoa wakati tuna ligi yetu.
Halafu mlivyo na dharau sisi tunalalama nyie hamtujibu chochote.
 
Ingekuwa ni wakati mzuri kwa Zanzibar kupitia baraza la wawakilishi kuona faida kuwa Michezo iwe jambo la Muungano kwa faida ya wanamichezo wa Zanzibar na hata kungekuwa na ligi moja ya Ya mpira wa miguu. Lakini sabbu ya unafiki na ulafi wa wanasiasa wataangalia zaidi faida za matumbo yao..
Zanzibar kamwe haiwezi kupewa unachama kwa kuwa kwa vigezo vya FIFA, sio nchi bali ni sehemu ya Tanzania. FIFA inatambua members wa UN. Kuna exception ya United Kingdom kwa sababu za kihistoria. Hawataki tena kurudia kosa hilo.

Mgao wa hela ya FIAFA na mambo mengine inaweza kuwa ni local arrangement ndani ya TFF. Zanzibar iwe treated kama special zone na mgawo wao uwepo kikanuni.

Vinginevyo tutapiga sana kelele hadi kiama. Alipata uanachama wa CAf ukaja kufutwa na Rais wa sasa. Hiyo ingekuwa nhgao ya kuombea uanachama wa FIFA japo bado ingekuwa vigumu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingekuwa ni wakati mzuri kwa Zanzibar kupitia baraza la wawakilishi kuona faida kuwa Michezo iwe jambo la Muungano kwa faida ya wanamichezo wa Zanzibar na hata kungekuwa na ligi moja ya Ya mpira wa miguu. Lakini sabbu ya unafiki na ulafi wa wanasiasa wataangalia zaidi faida za matumbo yao..

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawawezi kukubali ligi moja hata siku moja.

Fikiria hao Mlandege au Small Simba wakacheze Kagera, waende, Mtwar halafu waende Mbeya. Zanzibar na udogo wake wanashindwa itakuwa Tanganyika?

Njia nyingine wafikirie kugombea nafasi ndani ya TFF japo ni wazi uwezekano wa kupenya ni sawa na sifuri.
 
Zanzibar watapata pesa ya fika kama vyama vya michezo vya mikoa mingine vinavyopata kama Tanga au Arusha kudai wapate sawa kwa sababu wana ligi yao ni hoja ambayo ni ya kisiasa zaidi kwani kiukubwa ni sawa na mkoa mmoja wa Tanganyika sasa wapiganie wapate uanachama wao
 
Zanzibar kamwe haiwezi kupewa unachama kwa kuwa kwa vigezo vya FIFA, sio nchi bali ni sehemu ya Tanzania.
Kama ni hivyo basi hela iliyotolewa na FIFA ni ya Tanzania na hivyo TFF wanatakiwa kuwapa fungu lao, na FIFA hawawezi kuwa na tatizo. Wawape mgao wao. Yaani kwenye hela wanakuwa tena hawtambuliki kivipi sasa?
 
Hawawezi kukubali ligi moja hata siku moja.

Fikiria hao Mlandege au Small Simba wakacheze Kagera, waende, Mtwar halafu waende Mbeya. Zanzibar na udogo wake wanashindwa itakuwa Tanganyika?

Njia nyingine wafikirie kugombea nafasi ndani ya TFF japo ni wazi uwezekano wa kupenya ni sawa na sifuri.
Nafikiri huo ndio utakuwa wajibu wa mdhamini, kuziwezesha club kufika kila mahali kwani Namungo wanapotoka Lindi mpaka kagera nani anawawezesha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakinyimwa watafanyaje ,wakipeleka malalamiko FIFA hawatambuliwi huko

Back
Top Bottom