Zanzibar wanatumia mpira wa miguu kunung'unika.

Jibu hilo hapo chini
 
Hii shida haitokwisha bila kukubali katiba ya Mzee warioba. CCM wanajifanya kutoelewa lakini ni sawa na kufunika moto kwa blanket, moto utakuja kuwaka tu tunauchelewesha tu. Wanzanzibari hawatokubali kuendelea kukosa baadhi ya haki zao kama hiyo migao ya FIFA simply because hawatambuliki.

Mi sielewi kwa nini CCM wanaogopa Serikali tatu, hili ndo suruhisho pekee la kupata muungano wenye nguvu. Hata wazanzibari mwenyewe wengi wanapenda muungano lakini wanapenda wawe huru. Sijui mwisho wake nini kuendelea kushikilia watu kwa kutumia mabavu huku wenyewe hawaridhiki.
 
Hata Marekani kama watapewa fursa leo ya kuujadili muungano wao utavunjika. Waingereza walipewa fursa hiyo ya kuujadili muungano wa Ulaya, ona kilichotokea. Ona kule Catalonia Hispania kilichotaka kutokea. Muungano haujadiliwi, unaboreshwa humo kwa humo ndani kwa ndani. Siri kubwa ya kudumu kwa muungano ni kuongeza uhuru kwa wanandoa kujiamulia mambo yao madogomadogo ya kila siku.
 
Usifananishe Muungano wa marekani na huu wa Tanzania, Au Ujerumani na Tanzania.
Wenzetu Kila nchi ina Serikali yake Na Mamlaka yake, halafu ndio kuna Serikali ya Muungano ambayo nayo ina Madaraka yake na hayaingiliani. Ndio maana ukaona Marekani kama United States wanaruhusu ndoa za jinsia moja. Lakini humo marekani kuna nchi ambazo wamepiga marufuku, na Adhabu ya kifo ni Hivyo hivyo.
Wazanzibari hawajasema hawautaki Muungano, wazanzibari wanataka Muungano wa Haki. Kwanza ijitokeze Hiyo Serikali ya Tanganyaika, ijuilkane chanzo chake cha Mapato. Halafu ndio tuseme Hii ndio hiyo Serikali ya Muungano na itaendeshwa vipi? Sio kufanya Mambo kiujanja ujanja hivi, kua hiyo hiyo ni serikali ya Tanganyika wakati huo huo ni ya Muungano.
Munakataa nini? Semeni tu huu ni Ukoloni. Na Wazanzibari wanaelewa hilo tu
 
Halafu unaweza kukuta wakati unaandika haya yote upo bara,nyie wapemba akili zenu mnazijua wenyewe!
 
Na hata SIJUWI sababu ya WAZANZIBAR kuita Wa Tanganyika MACHOGO,,
 
Dawa halisi ya muungano ni serikali ya majimbo yanayojiendesha kwa aina fulani, hivyo kutakuwa na jimbo la Tanga lenye mikoa kadhaa, jimbo la Zanzibar, n.k. vinginevyo huu muungano tulionao sasa ni kiinimacho kweli, unadumishwa kwa mbinde, mizengwe na gharama kubwa za kificho na za waziwazi.

Unaonaje kama Rais na Makamu wake na waziri Mkuu wote wangekuwa wanatoka tanganyika? Kuna kujifunza kwingi sana kunakotuchelewesha sana kama Rais au Makamu atatokea Zanzabar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…