Zanzibar wapendekeza Tanganyika kuwa huru

Zanzibar wapendekeza Tanganyika kuwa huru

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
Na Ussi Talib

Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba Wilaya ya Kati Unguja, wamependekeza Katiba ijayo itamke rasmi kuwa mshirika wa Muungano ni Tanganyika na siyo Tanzania bara.

Maoni hayo yalitolewa jana huko Dunga wilayani humo mbele ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania inayongozwa na Mwenyekiti,Awadhi Ali Said.

Makame Ali Makame,alisema ikiwa Tanzania imekusudia kuondoa kero za muungano basi irudi katika uasilia wake wa nchi mbili huru zilizoungana ambazo ni Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar.

"Sawa na kukubaliana na mfumo mpya wa Muungano lakini Zanzibar iitwe hivyo na Tanganyika iitwe hivyo kama ilivyokuwa zamani" alisema Makame.

Pia aliitaka rasimu kila sehemu inayotaja Tanzania Bara itamke Tanganyika kwani kuweka kinyume na hivyo ni kumpa nafasi mmoja kujiona mkubwa.

Abuubakar Ussi Fadhili yeye alisema ni vyema kuweka uwazi huo ili kuondoa matatizo ambayo yanaweza kujitokeza.

Sambamba na hilo kwa upande wa Amin Yusouf Mussa mambo ya muungano yamependekezwa kuwa saba.

"Leo tunapendekeza mambo saba ya Muungano lakini Tanganyika haipo kama ikija kuyataka itakuwaje?"alihoji Mussa.

Akitoa ufafanuzi Mwenyekiti wa Kamati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Zanzibar,Awadhi Ali Said alisema,ili yatekelezeke hayo tume itaweka wazi shughuli za upande wa Tanzania bara ambazo zilikuwa zinashughulikiwa na Serikali ya Muungano na kuunda chombo chake kuyashughulikia.

Wajumbe hao wa Kamati ya mabadiliko ya Rasimu ya Katiba Mpya, wametawanyika katika sehemu mbalimbali kwa lengo la kukutana na wajumbe wa mabaraza ya Katiba walioteuliwa kuwakilisha wananchi ili kuunda Katiba Mpya itakayoleta mabadiliko ya mfumo na muundo mzima wa uongozi, watu na mamlaka husika kwa manufaa ya wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

Chanzo - Mwananchi
 
Sioni Kama ni tatizo Tanganyika ikiendelea kuitwa Tanzania ama Tanzania bara hata kama tutakua na katiba inayo tambua serikali tatu!
 
Afadhali maana watanganyika wenyewe wameshindwa kujitetea.
 
ni maoni yao tu tunaendelea kutoa maoni yetu.
 
Na Ussi Talib

Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba Wilaya ya Kati Unguja, wamependekeza Katiba ijayo itamke rasmi kuwa mshirika wa Muungano ni Tanganyika na siyo Tanzania bara.

Maoni hayo yalitolewa jana huko Dunga wilayani humo mbele ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania inayongozwa na Mwenyekiti,Awadhi Ali Said.

Makame Ali Makame,alisema ikiwa Tanzania imekusudia kuondoa kero za muungano basi irudi katika uasilia wake wa nchi mbili huru zilizoungana ambazo ni Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar.

“Sawa na kukubaliana na mfumo mpya wa Muungano lakini Zanzibar iitwe hivyo na Tanganyika iitwe hivyo kama ilivyokuwa zamani” alisema Makame.

Pia aliitaka rasimu kila sehemu inayotaja Tanzania Bara itamke Tanganyika kwani kuweka kinyume na hivyo ni kumpa nafasi mmoja kujiona mkubwa.

Abuubakar Ussi Fadhili yeye alisema ni vyema kuweka uwazi huo ili kuondoa matatizo ambayo yanaweza kujitokeza.

Sambamba na hilo kwa upande wa Amin Yusouf Mussa mambo ya muungano yamependekezwa kuwa saba.

“Leo tunapendekeza mambo saba ya Muungano lakini Tanganyika haipo kama ikija kuyataka itakuwaje?”alihoji Mussa.

Akitoa ufafanuzi Mwenyekiti wa Kamati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Zanzibar,Awadhi Ali Said alisema,ili yatekelezeke hayo tume itaweka wazi shughuli za upande wa Tanzania bara ambazo zilikuwa zinashughulikiwa na Serikali ya Muungano na kuunda chombo chake kuyashughulikia.

Wajumbe hao wa Kamati ya mabadiliko ya Rasimu ya Katiba Mpya, wametawanyika katika sehemu mbalimbali kwa lengo la kukutana na wajumbe wa mabaraza ya Katiba walioteuliwa kuwakilisha wananchi ili kuunda Katiba Mpya itakayoleta mabadiliko ya mfumo na muundo mzima wa uongozi, watu na mamlaka husika kwa manufaa ya wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

Chanzo - Mwananchi

Habari iendane na kichwa cha habari. Kwani Tanganyika sio huru?
 
Nakubaliana nao. Kiukweli Watanganyika walio wengi katika hili hatujui tulipo wala tunachotakiwa kukitetea. Tunaambiwa zinapendekezwa serikali tau, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ya Mapinduzi Zanzibar na ya Tanzania Bara...tunaona ni sawa tu. Yaani tupo tupo tu hata hatufikiri zaidi ya hapo. Ni kwanini wazanzibari hawataki ya kwao iitwe ya Tanzania Visiwani? Aksanteni wazanzibari katika hili la kutupigania nimewakubali.
 
Hii ni sawa na kukojolea nyaya za umeme. muungano ukikatika hakuna atakayesalimika.
 
Saafii sana wanznz kwa kuwafumbua macho watanganyika walisio na baba(katiba)
 
Hakuna mzanzibari hata wa kusingiziwa atakayekuewa endapo utasema zanzibar iitwe tanzania visiwano, kwa misingi hiyo, japo huku bara ukimtoa mch. Mtikila na kina sisi, walio wengi hawaoni shida kuitwa tanzania bara, ni vizuri na italeta tafsiri ya uasilia wetu kua na zanzibar na Tanganyika (ukipenda kuiita jamhuri sio mbaya) kama washirika wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ili kufanya trans-equity ya Wana muungano.
 
Wazanzibar wamekomaa kisiasa kuliko watanganyika!Uoga unatuponza.Zanzibar hakuna unafiki wanatamka waziwazi.Jaji mark bomani alitamka wazi kuitambua Tanganyika
 
Back
Top Bottom