Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

Wewe ndiyo umeingiza udini/uislamu hapo.Watanzania jumlisha na wazanzibari ni watu wasiopenda kufanya kazi kiuweledi zaidi.Na si hivyo tu.Wana viburi,kuzira na kutonyenyekea vyanzo vya mikate yao.Kwa kiingereza wanaitwa "wagaya siida"/hawapendi shida,kuulizwaulizwa wala kusumbuliwa na kusumbua akili zao.Meneja na his coy hapo hotelini wametudhihirishia tabia hizo halisi za watanzania wengi.
 
Watu wanajisahau sana, kama hawakupendezwa na hilo wangehama hoteli kimyakimya na sio kuanzisha fujo. Upo nchi za watu unataka kupangia watu maisha?
India kuna mtalii mwanamke muisrael raia wa Australia akakuta bango la kutetea wapalestina akalichana na kuanza kugombana na wenyeji.
Polisi wakamweka ndani rumande akafikishwa mahakamani katoka kwa dhamana bado kesi inaendelea.

Ni Kama ndugu zetu waisrael hawataki uhuru wa mawazo kuhusu mgogoro wa Gaza, wanataka wote dunia nzima isimame upande wao.
Wanahisi wana nguvu ya kulazimisha itikadi yao kote.
 
Hivi unafikiri meneja wa hoteli ni mjinga awafukuze watu waliolipia siku nyingi bila refund? Acha tu kuwatimua, hukusoma walienda kufanya fujo mapokezi kwa kulalamikia hilo gari lenye bendera za Palestina?
Wao walikuwa concerned na usalama wao .Sababu pale ni hoteli .Ina maana walipoingia hawakuona kitu kama hicho .Yawezekana huyo meneja baada ya kuona kuna waisrael hapo na ukereketwa wake wa kidini akaenda kuandika gari yake Free Palestine kwa makusudi ya kuwasuta au kuwapa mipasho hao wateja wake wayahudi.Hotel sio sehemu ya mwenye hotel au meneja kuwasuta au kuwapa mipasho wateja wake.Alichokifanya ni kuwapa mipasho na kuwasuta wateja wake kwa maandishi kwenye eneo la kupaki magari.Kibiashara haiko sahihi
 
H


Hata Marekani Kuna watu wanavaa tisheti zimeandikwa free palestine, wakati fulani free Mandela. Hiyo sio tatizo, ingekuwaje wangekuta mtu kaweka bendela ya Israel kwenye gari lake wangelalamika
Labda kama bango lemewekwa hotelini hiyo sio sawa
Kulikuwa na muda wa kuwaelewesha hao watalii na siyo kuwafurusha.
 
Hiyo ni sehemu ya biashara.Hatumchukui Ashura au Joni asiye na mafunzo ya kukirimu wateja kiuweledi.Sasa kuna haja gani ya kupeleka watu vyuo vya mambo ya uongozi mahiri wa hoteli kama huduma zenyewe siyo pursuasive kama hizo?Huduma zitolewapo zina miongozo/rules.And,rules are rules.Withou rules we are all savages!Ndiyo hapo tunafikia kufurusha wageni hotelini.
 
Hamuwajui Israel na hamjawahi kutana na kero zao, omba usikutane nazo... Wanaweza zua jambo dogo tu na kuanza kulalama pasipo na sababu ya msingi... Wanapenda sana refund, yaani sana
Nimemuandikia Nifah hapo chini kuhusu kufanya kazi kiuweledi. Please,soma kidogo.
 
Mbona kwenye mabasi mmetujazia mabendera ya israeli utadhani tupo Tel aviv au mnafikiri kila mtu anawapenda hao majambazi?
Ni bendera tu hazina maneno yeyote .Hilo gari lingekuwa na bendera tu bila maneno tena iko ndani ya gari wasingelalamika

Shida hayo maneno.Sasa mfano una tension ya kukodisha unaweka bingo free Palestine. Hivi unategemea nini?

Magari mengi hata maduka huwa na maneno ya dini lakini ya heri sio shari ya kivita.Maneno kama Mungu bariki biashara yangu nk

Kuweka hayo ya Free Palestine hapana
 
Hotel au sehemu yenye kutoa huduma kwa watu wenye itikadi,imani,maono mchanganyiko unawekaje vitu vitakavyowakwaza?Kutokujielewa huko na kuharibu biashara.
Ndugu yangu we, sioni kosa la meneja wa hotel. Ulaya na dunia yote kuna maandamano na kelele nyingi za kutaka Israel iache kukandamiza wapelestina. By the way mbona maandishi na kampeni za kuunga mkono ushoga zimewekwa kila mahali kwenye hotel kubwa majuu? Unafikiri mtu mwenye msimamo tofauti ukienda pale na kuhoji watakuchekea?
 
Kama ulishawahi fanya kazi na waisrael, hapa utajua na utaelewa ni nani mwenye kosa
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Unavyowaeleza na kutuchorea picha za hao jamaa vichwani mwetu utadhani ni mashetani fulani hivi.Hata mimi,zamani hizo nilijengewa picha mawazoni mwangu kwamba wahindi ni wasumbufu,wenye dharau na hupenda kutumatuma bila kuzingatia ustaarabu.
 

Manager is a neutral point, Hotel inahudumia wato wote, hapaswi ku engage na hayo Mambo, ni Mpumbavu kabisa.
 
Hivi,ukikaa kwa kutulia ukajiuliza,ni watoto wa kipalestina tu ndiyo pekee wanaokufa kwa mapigano hapa duniani?Umeitazama DRC?Umeiona Sudan?Chad?Ukraine?Lakini,kelele nyingi nazo humuokoa mke kutoka kwenye kipigo cha mumewe!
 
Kumbe wewe huna akili sasa kusapoti palestina iwe huru ni kosa? Wewe hautaki palestina iwe huru dhidi ya ukandamizaji unaofanywa na israeli?
 
Nimemuandikia Nifah hapo chini kuhusu kufanya kazi kiuweledi. Please,soma kidogo.
Bro najishughulisha na kazi za utalii, nishafanya kazi hotelini.. niamini, hapo waisraeli ndio wenye shida,

Siku zote Manager ama mfanyakazi lazima asikilize kero ya mteja kwenye hii sekta, changamoto inakuja pale ambapo unakutana na wateja ambao si waelewa kama waisrael, muda wote wanalilia redund (wanaongoza katika hili)... Wao wanajiona wapo perfect muda wote na wanataka kuogopwa na kunyenyekewa...

Nina uhakika hapo waliomba refund, na wakiona haiwezekani hulalamika wanaonewa, na si ajabu ni wao ndio waliochapisha hiyo habari mtandaoni
 


It has to cause them concern, wao wana passport ya Israel, kwa Mtazamo wao, Free Palestinian means from Israel, na host wao ambaye ni Manager anaona wao sio fair, it has to raise concern.
 
Hakuna ubaya wowote. Pengine suala la Palestina vs Israel wewe hulijui au unalijua kwa mtizamo wa kidini. Kwa taarifa yako haya maneno ni slogan ya nchi nyingi duniani na hata Umoja wa Mataifa. Huyo meneja apewe maua yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ