JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Watoto watatu wamefariki dunia na wengine 316 wamethibitika kuugua ugonjwa wa surua katika kipindi cha mwezi mmoja visiwani Zanzibar.
Wilaya ya Magharibi B Unguja inaongoza ikiwa na vifo viwili na zaidi ya watoto 200 wamebainika kuwa na surua. Wilaya ya Magharibi A ina wagonjwa zaidi ya 70 na Wete zaidi ya 40.
Meneja Kitengo cha Elimu ya Afya, Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Bakari Hamad Magarawa amesema, “kuna wilaya chache ambazo hazijaripoti ugonjwa huo, natoa wito tuwapeleke watoto wakachanje chanjo ya surua.
“Chanjo ni bure, inatolewa kuanzia miezi 9 na inarudiwa baada ya mwaka mmoja na nusu.”
Source: Azam TV