figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,132
- 64,416
Wakuu,
Kuna habari zinadai kwamba kuna Wavuvi watatu, hawajulikani walipo na hii ni siku ya 10.
Je, watakuwa wapi? Au wamekamatwa?
Tunaomba wenye details juu ya hii stofahamu asaidie kupatikana kwa hawa watu.
Stay tuned
=====
Serikali yaombwa kusaidia kutafuta miili ya Wavuvi watatu waliozama bahari kuu siku kumi zilizopita.
Akiongea na JamiiForums, mmoja wa ndugu wa waliozama bahari amesema kwamba, Wavuvi hao walienda kuvua samaki bahari kuu wakiwa watatu, siku hiyo bahari ikachafuka na kukawa na upepo mkali uliosababisha boti yao kuzama.
Ameongeza kwamba wakati wanazama, walikuwa na wavuvi wengine waliokuwa bahari kuu lakini kutokana na upepo kuwa mkali walishindwa kuwaokoa
Hivyo ndugu wameomba Serikali kusaidia kutafuta kwani mara nyingi watu wakizama, wanaokototwa Kenya Somalia au Comoro. Hivyo wameomba Serikali iwasaidie kutafuta na kupata miili ya wapendwa wao katika nchi hizo.
Wametajwa waliozama kuwa ni Abdallah Hamis, Mwadini Bakari na mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Ismail. Wote ni Wakazi wa Kijiji cha Mtangani Wilaya ya Mkoani na Mkoa wa Kusini Pemba Zanzibar