Zanzibar yaandaa Bonanza la Utalii, Michezo na Utamaduni la Pemba, tarehe 27 hadi 30 Novemba 2024

Zanzibar yaandaa Bonanza la Utalii, Michezo na Utamaduni la Pemba, tarehe 27 hadi 30 Novemba 2024

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Salaam Wakuu,

Zanzibar yaandaa Bonanza la Utalii, Michezo na Utamaduni la Pemba, tarehe 27 hadi 30 Novemba 2024.

Hapa chini ni Hotuba iliyotolewa leo na Mhe. Mudrik R. Soraga Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale kuelekea Bonanza hilo.

======

HOTUBA KWA UZINDUZI WA PEMBA TOURISPORT AND CULTURAL BONANZA (PTCB24)


Ndugu Katibu Mkuu, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale

Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar

Viongozi na wadau wa sekta ya utalii, ZATO, ZATI, HAZ, ZNCC

Wadau wa maendeleo,

Wageni waalikwa, na wanahabari,

Assalam Aleykum

Ndugu zangu, tunakutana hapa leo kwa lengo la kuanzisha hatua mpya ya kimkakati kuelekea Bonanza la Utalii, Michezo na Utamaduni la Pemba, Pemba Tourisport and Cultural Bonanza (PTCB), linalotarajiwa kufanyika rasmi kuanzia tarehe 27 hadi 30 Novemba 2024. Uzinduzi huu unalenga kuleta uelewa kwa wadau wote juu ya tukio hili muhimu, pamoja na kufafanua nafasi muhimu ambayo Bonanza hili litachukua katika kutangaza na kukifungua kisiwa cha Pemba kimkakati kama kitovu cha utalii.

PTCB 2024 ni Bonanza la sita, na kila mwaka Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ongezeko la washiriki kutoka maeneo tofauti ikiwemo Tanzania bara na nchi jirani, kufanya maboresho katika matukio hayo, na kutangaza zaidi vivutio vya kisiwa cha Pemba kwa hadhira ya kimataifa zaidi.

Bonanza hili linaendelea kuboresha taswira ya Pemba kimataifa kama kituo cha michezo, urithi na utalii endelevu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Awamu ya Nane chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Kwa nini Utalii wa Michezo kwa Pemba?

Utalii wa Michezo una nafasi kubwa katika kuongeza hamasa, kushawishi vijana na jamii kushiriki, na kuvutia watalii wa ndani na nje. Michezo itakayofanyika kwenye PTCB ni pamoja na:

1. Triathlon – kuongelea, kuendesha baiskeli, na kukimbia

2. Mashindano ya Ngalawa

3. Mashindano ya kuogelea

4. Gwaride la Punda

5. Mchezo wa Ng'ombe

6. Duathlon – kuendesha baiskeli na kukimbia mbio

Matokeo Yanayotarajiwa

Lengo ni kuitambulisha na kuifungua Pemba kama kitovu cha Utalii wa Kijani unaolenga katika kuhamasisha Michezo, urithi, na Utamaduni wetu. Hii ni pamoja na:

• Kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Kisiwa cha Pemba.

• Kukuza uchumi wa Pemba kwa kupitia ajira na shughuli za kitalii.

• Kuvutia wawekezaji katika utalii wa michezo, urithi na afya na kuchochea miundombinu inayoendana na utalii endelevu.

Tunatoa wito kwa wadau wote kushiriki kikamilifu na kuchangia kwenye PTCB 2024, ili tuweze kujenga na kuifungua Pemba mpya, inayotambulika kimataifa kwa vivutio vyake vya kipekee na ushawishi mkubwa katika utalii wa michezo na utamaduni.

Asanteni sana kwa kuhudhuria uzinduzi huu, na tuna matumaini ya ushirikiano wenu katika kufanikisha Bonanza la mwaka huu.

Hitimisho

PTCB ni ramani kwa ajili ya kuitangaza Pemba kimkakati katika uwanja wa Utalii, Michezo na Utamaduni Kitaifa, Kikanda na Kimataifa. Na shughuli nyingi zilizopangwa katika maeneo ya Pemba, Bonanza hili linatoa wigo wa uzoefu tofauti. Kamisheni ya talii ya Zanzibar inawaalika wadau wote wanaoweza kuungana nasi katika kufanikisha PTCB 2024.

Vilevile napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Baraza la Taifa la Michezo

Zanzibar na wadhamini wetu kwa mwaka huu;

• ZURA

• Tigo/ Zantel – Ofisi ya Pemba

• Pemba Water

Fomu za kushiriki michezo hiyo zinapatikana Kamisheni ya Utalii Zanzibar.
DSC07782.jpeg
DSC07818.jpeg
DSC07815.jpeg
DSC07826.jpeg
DSC07833.jpeg
DSC07856.jpeg
DSC07867.jpeg
DSC07877.jpeg
DSC07881.jpeg
DSC07888.jpeg
DSC07891.jpeg
DSC07895.jpeg
DSC07896.jpeg
DSC07898.jpeg
DSC07907.jpeg
DSC07900.jpeg
DSC07933.jpeg
DSC07956.jpeg
DSC07980.jpeg
DSC07996.jpeg
DSC07994.jpeg
DSC08007.jpeg
DSC08014.jpeg
DSC08041.jpeg
DSC08113.jpeg
DSC08130.jpeg
DSC08007.jpeg
 

Attachments

  • DSC08007.jpeg
    DSC08007.jpeg
    680.2 KB · Views: 4
Back
Top Bottom