Zanzibar yaanzisha bima kwa wageni (US$44), kuanzia kutumika Septemba 1, 2024

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Zanzibar: Bima kwa wageni watalii US$44 kuanza 1 September 2024

Mkuya.jpg

Dk. Saada Mkuya Salum

WAZIRI wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum amesema uwepo wa bima ya wasafiri kutaongeza kasi ya idadi ya watalii kufika Zanzibar na serikali kupata mapato yatokanayo na sekta ya utalii.

Aliyasema hayo jana wakati wa utambulisho wa bima hiyo kutoka kwa wadau wa sekta ya usafiri.

Alisema Serikali ya Zanzibar inatarajia kuweka bima ya wasafiri kwa wageni wanaofika Zanzibar ambapo bima hiyo itaanza rasmi mwanzoni mwa Septemba mwaka huu.

Alisema serikali inaendelea na kukamilisha taratibu ya bima hiyo ambao itasimamiwa na Shirika la Bima Zanzibar na itasiadia kuhudumia wageni.

Aidha, alisema pia serikali inaendelea kuboresha miundombinu yao ya kiuchumi pamoja na mifumo ili kuhakikisha wanatoa huduma bora wa wananchi pamoja na wageni.

Hivyo, alisema serikali itajitahidi kuweka miundombinu ambayo itahakikisha wananchi na wageni wanapata huduma bora na wanaendelea na mchakato kuona mambo yao yanakuwa mazuri ili watakapoanza kutumia huduma hiyo kuwe hakuna changamoto.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC), Jape Ussi Khamis, alisema uwepo wa bima hiyo itachangia utalii kuwa mzuri na Zanzibar kuwa salama kwa watalii wanaoitembelea.

Alisema kuwa serikali inatengeneza mambo mengi mazuri kwa ajili ya uchumi wa Zanzibar na miongoni mwa suala ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi ni sekta ya utalii.

Meneja Biashara, Benki, Bima, Mawakala na Mauzo kutoka ZIC, Hamida Salim Juma alisema bima ya usaifri ni sawa na bima nyingine ambazo mgeni ataipata akiwa nchini na itaukuza uchumi wao na kuupa tija.

Alisema bima hiyo haitatumika katika masuala ya kiafya pekee bali itatumika kwa majanga yote ambayo watakuwa wanapata wageni hao wakiwa nchini au katika mipaka ya Tanzania.

Alisema utaratibu wa kupata bima hiyo utaanzia tangu mgeni huyo atakapoomba kufika Zanzibar.
 
24 July 2024​

Zanzibar to Introduce Inbound Health Insurance​

Zanzibar to introduce Inbound Health Insurance of $44pp from 1st September 2024.

Foreign visitors (maybe excl EAC nationals), will be covered medically locally, or in some cases even Air Transferred to Nairobi Kenya or Madrid Spain depending on the need of medical attention, maybe once cover is triggered it covers you within 14 days or 1st 14 days but the Government of Zanzibar hasn't specified yet.

Inbound health insurance has been an option in other countries, such as Saudi, and recently become part of visa for those visitors, staying longer than certain period, for example in the United Kingdom - UK etc

Its suppose to be compulsory, to all non-Tanzania nationals, At checkin for departures to Zanzibar, you must present the new Inbound Medical Insurance proof or pay at checkin. In some cases evacuation to your home country is included.
 
24 July 2024
Unguja, Zanzibat

Zanzibar bima kwa wageni watalii US$44 kuanza 1 September 2024

Waziri wa fedha wa SMZ Dr. Saada Mkuya atangaza mtalii na wageni wasio raia wa Tanzania anatakiwa kuwa na bima ya lazima Inbound Travel Insurance

Kabla ya kupanda ndege kuja Zanzibar sasa mgeni na mtalii kutoka nje mbali ya passport, visa atatakiwa kuonesha bima hiyo kabla ya kuruhisiwa kupanda ndege huko atokako. Hii ni lazima kwa kuwa ni takwa la kisheria Zanzibar.

Naye meneja wa biashara na mauzo wa shirika la bima Zanzibar (ZIC) bi. Hamida Salum Juma amefafanua zaidi kuwa bima hiyo haitamfunga mtalii au mgeni atibiwe Zanzibar tu, bali hali halisi itaangaliwa je mtalii au mgeni anaweza kupata huduma Zanzibar au kama haiwezekani bima hiyo itaweza kutumika nje mfano Nairobi Kenya au Madrid Spain ikiwa italazimika mgeni kupelekwa huko kutokana na hitaji hilo.

Bima hiyo ni ya kipindi cha siku 14 meneja wa ZIC Shirika la Bima Zanzibar amesema.
Hao raia wao wenyemewe wamewapa bima wote mpaka waanza kwa wageni?
 
Waseme covarage yake ikoje, isiwe kama NHIF inayobagua magonjwa. Tujue tukilipia tunaweza kusafirishwa kupata matibabu sahihi kwenye hospitali zenye huduma zote stahiki.
 
Wageni wengi huwa wanakuwa na bima kutoka nchini kwao ili wakiugua wapate tiba katika hospitali zinazoeleweka. Ina maana kuwa hata hawa watalazimika kununua Bima nyingine kutoka makampuni yaliyopo Zanzibar?

Amandla...
 
Swali la nyongeza,shirika la bima Zanzibar ZIC, Ma ajenti wao huko nje watakuwa kina nani au ZIC itakwenda online kurahishisha mambo www.zic.co.tz

1721913872406.png

More info :

1721914287391.png

Travel insurance is a great way to protect your financial investment for your trip. Travel benefits can provide coverage for prepaid, non-refundable trip costs and some plans also offer limited medical benefits
 
24 July 2024
Unguja, Zanzibat

Zanzibar bima kwa wageni watalii US$44 kuanza 1 September 2024

Waziri wa fedha wa SMZ Dr. Saada Mkuya atangaza mtalii na wageni wasio raia wa Tanzania anatakiwa kuwa na bima ya lazima Inbound Travel Insurance

Kabla ya kupanda ndege kuja Zanzibar sasa mgeni na mtalii kutoka nje mbali ya passport, visa atatakiwa kuonesha bima hiyo kabla ya kuruhisiwa kupanda ndege huko atokako. Hii ni lazima kwa kuwa ni takwa la kisheria Zanzibar.

Naye meneja wa biashara na mauzo wa shirika la bima Zanzibar (ZIC) bi. Hamida Salum Juma amefafanua zaidi kuwa bima hiyo haitamfunga mtalii au mgeni atibiwe Zanzibar tu, bali hali halisi itaangaliwa je mtalii au mgeni anaweza kupata huduma Zanzibar au kama haiwezekani bima hiyo itaweza kutumika nje mfano Nairobi Kenya au Madrid Spain ikiwa italazimika mgeni kupelekwa huko kutokana na hitaji hilo.

Bima hiyo ni ya kipindi cha siku 14 meneja wa ZIC Shirika la Bima Zanzibar amesema.
Mbona kama ni njia ya kuwafukuza hao watalii?
 
Zanzibar isipokuwa makini, utalii na uchumi wake buluu utaanguka vibaya sana.

Maamuzi ya kisiasa bila kushirikisha wadau wanaofahamu sekta ya utalii na safari utaifanya Zanzibar kukosa umaarufu wake na wageni pia.

Kuna sehemu za utalii duniani (destinations) zitakazotoa ushindani kwa Zanzibar kama Sosua Dominican Republic, Jamaica, Barbados, Mauritius, Maldives, Thailand, Mombasa, Malindi n.k
 
Mkuu acha kuoanisha Thailand na Mauritius na vitu vya kijinga, hao watu wapo mbali sana hatustahiki kutajwa pamoja nao
 
Hii nchi ni ya kipuuzi sana, vichwa vya vipo katika kuengezea mzigo watalii tu, ni ngumu sana sisi kusogea mbele kwenye utalii
 
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imeanzisha travel insurance kwa kila mgeni ( foreigner ) atakayeingia Zanzibar kuanzia 1 Oct 2024, je hii ni sahihi au ni upungufu wa ubunifu wa kukuasanya kodi, maana sekta ya utalii pekee ndio inayobinywa, pengine hii kutaifanya Zanzibar kua ni expensive and unaffordable travel destination, kumbuka kua, Zanzibar kila mgeni akiingia anachajia infrastructure fees ambayo ni per person per night.

Nawakilisha
 
Nahisi walengwa ni wale wanaotoka nchi ya kusadikika ili watimuliwe toka zenji kuwa hawana bima
 
Zanzibar: Bima kwa wageni watalii US$44 kuanza 1 September 2024

View attachment 3074939

Dk. Saada Mkuya Salum

WAZIRI wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum amesema uwepo wa bima ya wasafiri kutaongeza kasi ya idadi ya watalii kufika Zanzibar na serikali kupata mapato yatokanayo na sekta ya utalii.

Aliyasema hayo jana wakati wa utambulisho wa bima hiyo kutoka kwa wadau wa sekta ya usafiri.

Alisema Serikali ya Zanzibar inatarajia kuweka bima ya wasafiri kwa wageni wanaofika Zanzibar ambapo bima hiyo itaanza rasmi mwanzoni mwa Septemba mwaka huu.

Alisema serikali inaendelea na kukamilisha taratibu ya bima hiyo ambao itasimamiwa na Shirika la Bima Zanzibar na itasiadia kuhudumia wageni.

Aidha, alisema pia serikali inaendelea kuboresha miundombinu yao ya kiuchumi pamoja na mifumo ili kuhakikisha wanatoa huduma bora wa wananchi pamoja na wageni.

Hivyo, alisema serikali itajitahidi kuweka miundombinu ambayo itahakikisha wananchi na wageni wanapata huduma bora na wanaendelea na mchakato kuona mambo yao yanakuwa mazuri ili watakapoanza kutumia huduma hiyo kuwe hakuna changamoto.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC), Jape Ussi Khamis, alisema uwepo wa bima hiyo itachangia utalii kuwa mzuri na Zanzibar kuwa salama kwa watalii wanaoitembelea.

Alisema kuwa serikali inatengeneza mambo mengi mazuri kwa ajili ya uchumi wa Zanzibar na miongoni mwa suala ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi ni sekta ya utalii.

Meneja Biashara, Benki, Bima, Mawakala na Mauzo kutoka ZIC, Hamida Salim Juma alisema bima ya usaifri ni sawa na bima nyingine ambazo mgeni ataipata akiwa nchini na itaukuza uchumi wao na kuupa tija.

Alisema bima hiyo haitatumika katika masuala ya kiafya pekee bali itatumika kwa majanga yote ambayo watakuwa wanapata wageni hao wakiwa nchini au katika mipaka ya Tanzania.

Alisema utaratibu wa kupata bima hiyo utaanzia tangu mgeni huyo atakapoomba kufika Zanzibar.
Mkuu huu ni udhubutu wa kupigwa na ubunifu mzuri. Hongereeni sana!
 
Back
Top Bottom