Hao raia wao wenyemewe wamewapa bima wote mpaka waanza kwa wageni?24 July 2024
Unguja, Zanzibat
Zanzibar bima kwa wageni watalii US$44 kuanza 1 September 2024
Waziri wa fedha wa SMZ Dr. Saada Mkuya atangaza mtalii na wageni wasio raia wa Tanzania anatakiwa kuwa na bima ya lazima Inbound Travel Insurance
Kabla ya kupanda ndege kuja Zanzibar sasa mgeni na mtalii kutoka nje mbali ya passport, visa atatakiwa kuonesha bima hiyo kabla ya kuruhisiwa kupanda ndege huko atokako. Hii ni lazima kwa kuwa ni takwa la kisheria Zanzibar.
Naye meneja wa biashara na mauzo wa shirika la bima Zanzibar (ZIC) bi. Hamida Salum Juma amefafanua zaidi kuwa bima hiyo haitamfunga mtalii au mgeni atibiwe Zanzibar tu, bali hali halisi itaangaliwa je mtalii au mgeni anaweza kupata huduma Zanzibar au kama haiwezekani bima hiyo itaweza kutumika nje mfano Nairobi Kenya au Madrid Spain ikiwa italazimika mgeni kupelekwa huko kutokana na hitaji hilo.
Bima hiyo ni ya kipindi cha siku 14 meneja wa ZIC Shirika la Bima Zanzibar amesema.
Wageni wengi huwa wanakuwa na bima kutoka nchini kwao ili wakiugua wapate tiba katika hospitali zinazoeleweka. Ina maana kuwa hata hawa watalazimika kununua Bima nyingine kutoka makampuni yaliyopo Zanzibar?
Amandla...
Watalii karibia wote wanakuja na bima zao kulingana na hali zao za afya na vipato!Baadhi ya watalii wanakata bima kwao kabla ya kuja Zanzibar
Mbona kama ni njia ya kuwafukuza hao watalii?24 July 2024
Unguja, Zanzibat
Zanzibar bima kwa wageni watalii US$44 kuanza 1 September 2024
Waziri wa fedha wa SMZ Dr. Saada Mkuya atangaza mtalii na wageni wasio raia wa Tanzania anatakiwa kuwa na bima ya lazima Inbound Travel Insurance
Kabla ya kupanda ndege kuja Zanzibar sasa mgeni na mtalii kutoka nje mbali ya passport, visa atatakiwa kuonesha bima hiyo kabla ya kuruhisiwa kupanda ndege huko atokako. Hii ni lazima kwa kuwa ni takwa la kisheria Zanzibar.
Naye meneja wa biashara na mauzo wa shirika la bima Zanzibar (ZIC) bi. Hamida Salum Juma amefafanua zaidi kuwa bima hiyo haitamfunga mtalii au mgeni atibiwe Zanzibar tu, bali hali halisi itaangaliwa je mtalii au mgeni anaweza kupata huduma Zanzibar au kama haiwezekani bima hiyo itaweza kutumika nje mfano Nairobi Kenya au Madrid Spain ikiwa italazimika mgeni kupelekwa huko kutokana na hitaji hilo.
Bima hiyo ni ya kipindi cha siku 14 meneja wa ZIC Shirika la Bima Zanzibar amesema.
Mbona kama ni njia ya kuwafukuza hao watalii?
Zanzibar isipokuwa makini, utalii na uchumi wake buluu utaanguka vibaya sana.
Maamuzi ya kisiasa bila kushirikisha wadau wanaofahamu sekta ya utalii na safari utaifanya Zanzibar kukosa umaarufu wake na wageni pia.
Kuna sehemu za utalii duniani (destinations) zitakazotoa ushindani kwa Zanzibar kama Sosua Dominican Republic, Jamaica, Barbados, Mauritius, Maldives, Thailand, Mombasa, Malindi n.k
Mkuu huu ni udhubutu wa kupigwa na ubunifu mzuri. Hongereeni sana!Zanzibar: Bima kwa wageni watalii US$44 kuanza 1 September 2024
View attachment 3074939
Dk. Saada Mkuya Salum
WAZIRI wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum amesema uwepo wa bima ya wasafiri kutaongeza kasi ya idadi ya watalii kufika Zanzibar na serikali kupata mapato yatokanayo na sekta ya utalii.
Aliyasema hayo jana wakati wa utambulisho wa bima hiyo kutoka kwa wadau wa sekta ya usafiri.
Alisema Serikali ya Zanzibar inatarajia kuweka bima ya wasafiri kwa wageni wanaofika Zanzibar ambapo bima hiyo itaanza rasmi mwanzoni mwa Septemba mwaka huu.
Alisema serikali inaendelea na kukamilisha taratibu ya bima hiyo ambao itasimamiwa na Shirika la Bima Zanzibar na itasiadia kuhudumia wageni.
Aidha, alisema pia serikali inaendelea kuboresha miundombinu yao ya kiuchumi pamoja na mifumo ili kuhakikisha wanatoa huduma bora wa wananchi pamoja na wageni.
Hivyo, alisema serikali itajitahidi kuweka miundombinu ambayo itahakikisha wananchi na wageni wanapata huduma bora na wanaendelea na mchakato kuona mambo yao yanakuwa mazuri ili watakapoanza kutumia huduma hiyo kuwe hakuna changamoto.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC), Jape Ussi Khamis, alisema uwepo wa bima hiyo itachangia utalii kuwa mzuri na Zanzibar kuwa salama kwa watalii wanaoitembelea.
Alisema kuwa serikali inatengeneza mambo mengi mazuri kwa ajili ya uchumi wa Zanzibar na miongoni mwa suala ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi ni sekta ya utalii.
Meneja Biashara, Benki, Bima, Mawakala na Mauzo kutoka ZIC, Hamida Salim Juma alisema bima ya usaifri ni sawa na bima nyingine ambazo mgeni ataipata akiwa nchini na itaukuza uchumi wao na kuupa tija.
Alisema bima hiyo haitatumika katika masuala ya kiafya pekee bali itatumika kwa majanga yote ambayo watakuwa wanapata wageni hao wakiwa nchini au katika mipaka ya Tanzania.
Alisema utaratibu wa kupata bima hiyo utaanzia tangu mgeni huyo atakapoomba kufika Zanzibar.
🤔Nahisi walengwa ni wale wanaotoka nchi ya kusadikika ili watimuliwe toka zenji kuwa hawana bima