Zanzibar yapiga marufuku ndoa za jinsia moja

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetunga sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja.Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Katika swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya Zanzibar itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali kwa watu ambao watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu. Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.

Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi yakiwemo ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana adhabu ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," mwisho wa kunukuu.
 
CUF wanapingana na sera za Kiliberali na wajitoe basi kwenye huo umoja wao
 
Duu watanzania huu unafiki mpaka lini cuf? Nataka sitaki! Wao mpaka usagaji! Watanzania tusiingia kichwa kwenye vyama hivi. Daah yaani Maana ya Haki sawa kwa Wote, kwamba mashoga na Wasagaji wote waheshimiwe! Kazi tunayo watz!
 
Kama sheria za Zanzibar tayari zinatamka kwamba "NDOA NI KATI YA MWANAMKE NA MWANAMME" basi hakuna swala la kukataza ndoa ya jinsia moja kwani hakuna kitu kama hicho. Na sheria ya ndoa ya Zanzibar lazima inatoa definition ya NDOA kwanza.

Sasa tunavuka mito ambayo haipo. Kinachofanyika kwa wenzetu ni KURUHUSU ndoa kati ya watu wa jinsia moja. Ni mbaya, lakini hakuna contradiction in terms kwani unaweza kuruhusu kitu ambacho kilikuwa kimekatazwa. Zanzibar wanakataza kitu ambacho kilikuwa kimekatazwa!
 
Hili suala litaleta shida sana

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Democrasia ndo chanzo cha ushoga duniani!!inchi zinazojidai kutetea haki za binadam na demokrasia km marekan,wingereza,ufaransa ndio zinazoongoza kwa ushenz wa ushoga na usagaji!!,

pia,zanzibar hakukua na uhuru wa ndoa ya jinsia moja,so mtoa mada ungesema kua zanzibar yatunga sheria kuzuia ndoa za jinsia moja,lkn ukisema yapiga marufu kwani hapo zamani iliruhusiwa?
 
CUF waache unafiki ukiamua kua moto kua moto kama baridi kua baridi tu na sio vuguvugu wao si Waliberali bwana na Waliberali wanaamini katika ndoa za jinsia moja au walikua hawajui wanajiunga na ninu?

The leader of the Liberal Democrats, Nick Clegg, supports same-sex marriage and has stated that his party backs its legalisation.On 4 July 2009 in an article for LabourList, Clegg wrote that "although civil partnerships have been a step forward, until same sex marriage is permitted it is impossible to claim gay and straight couples are treated equally." Following this, the party's LGBT equality body DELGA launched a petition "Marriage Without Borders" calling for all gender restrictions on marriage and civil partnerships to be lifted, and for same-sex relationships to be recognised across Europe and internationally(including Zanzibar). The petition was run at Manchester Pride and Reading Pride in 2009, and launched online in January 2010 following an interview with Clegg in Attitude magazine in which he reaffirmed his commitment to equal marriage. However this did not make it into the party's manifesto. In an interview in July 2010 Lib Dem deputy party leader Simon Hughes confirmed that the coalition government plans to open marriage to same-sex couples, saying, "It would be appropriate in Britain in 2010, 2011, for there to be the ability for civil marriage for straight people and gay people equally ... The state ought to give equality. We're halfway there. I think we ought to be able to get there in this parliament".


In 2010, at their spring conference the Scottish Liberal Democrats passed a motion calling on the Scottish Government to allow gay couples to marry, describing the exclusion of same-sex couples from marriage as a "discrimination that needs to end". In September 2010, the Liberal Democrats at their Autumn Federal Conference voted to make marriage equality a party policy at the Westminster level.
 
Vyama na makanisa yanayokumbatia ushoga yapigwe marufuku tanzania tukianzia na cdm
 
Huu upuuz wa CDM nadhan unalengo la kuchafuana na kuleta sintofahamu kwa wananchi. Sasa kama CUF ni chama cha kishoga kilipata vp usajili ikiwa Tanzania inapinga ushoga? Sasa naamin ya kwamba CDM ina watu MATAHIRA!!!
 

CUF kama wako serious na hilo basi wajiandae kufurushwa kutoka umoja wa nchi za kiliberali na hata wao wabadilishe kauli mbiu yao "HAKI SAWA KWA WOTE" kwa sababu wanahubiri wasichokitekeleza; watakuwa wameamua kuwatelekeza mashoga na wasagaji!!
 
Huu upuuz wa CDM nadhan unalengo la kuchafuana na kuleta sintofahamu kwa wananchi. Sasa kama CUF ni chama cha kishoga kilipata vp usajili ikiwa Tanzania inapinga ushoga? Sasa naamin ya kwamba CDM ina watu MATAHIRA!!!
HUJUI HISTORIA YA CUF.
1.CUF isajiliwa 1992
2.CUF ilijiunga na ULIBERALI 1997 ikiwa tayari ina usajili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…