Zanzibar yapiga marufuku upigaji wa makachu Forodhani hadi serikali itakapoandaa utaratibu maalum wa shughuli hiyo

Zanzibar yapiga marufuku upigaji wa makachu Forodhani hadi serikali itakapoandaa utaratibu maalum wa shughuli hiyo

Ilitakiwa watoe muongozo wa mavazi.

Tuseme jambazi limekimbilia msituni basi solution ni kuchoma msitu?

Sio kweli asee.
......kusimamisha kwa muda ili kutoa muongozp sasa....tuwape muda warudi...
 
ukishaamua kupata pesa za utalii jiandae na cosequence zake. ukianza tena kuweka mashart ni kama jela. tatizo la makachu pale ambalo mim niliona sio zur ni ku dive maji madogo. yakiwa hayajakupwa. ile mbaya
kusema watalii wasipige makachu mtakua hamjafikiriq vizur in economics ways. zile clips zinavosambqa dunian ni ajab sana unaweza kuta mtu aanapanda ndege just kuja kupiga makachu . haya upo taayri kupoteza hela.??
define kwaza vacation na tourism ndio mtajua mnaanzia wap nyie watu wa Mamlaka ya mji mkongwe.
 
Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar imepiga marufuku upigaji wa makachu katika eneo la bustani ya Forodhani baada ya kudaiwa kufanyika kwa matendo ambayo ni ukiukwaji wa maadili ya Zanzibar na kufanyika kwa baadhi ya uharibu katika eneo hilo

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kuona kuna ukiukwaji wa sheria, kanuni na miongozo yaliyojitokeza kwa vijana wa makachu katika eneo hilo ambapo inahusisha pia upigaji makachu kwa kutumia mavazi yanayokwenda kinyume na Utamaduni, Uharibifu wa mifereji na miundombinu mengine ikiwa ni pamoja na kutumia madebe taka kufanyia vichekesho (comedy).

Aidha mamlaka hiyo imesema imesimamisha shughuli hizo hadi kukamilika na kuandaa utaratibu wa kuimarisha utendaji kazi hizo kwani Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na vijana hao katika kuutangaza Utalii wa Zanzibar Kimataifa.

Vilevile Mamlaka hiyo inaendelea kufanya uchunguzi wa matukio hayo na kuwachukulia hatua wale wote waliobainika kutenda makosa hayo ikiwemo uharibifu wa miundombinu.

Hivi karibuni ilisambaa video ikionesha baadhi ya Raia ambao ni wa Kigeni kupiga makachu katika eneo hilo wakiwa na nguo ambazo haziendani na maadili ya Zanzibar.
Kwa jinsi navyoijua zanzibar hizi ni kelele za geresha tu. Hakuna hatua yoyote watakayochukua.
 
Back
Top Bottom