Elections 2010 Zanzibar yapingana na ZEC-CCM kura ya maoni na Mseto kabla ya uchaguzi mkuu

Elections 2010 Zanzibar yapingana na ZEC-CCM kura ya maoni na Mseto kabla ya uchaguzi mkuu

Niliwahi kusema katika thread nyuma kuwa ukisikia changa la macho ndio hili hivi inawezekana kweli ukasimamia daftari la uchaguzi huku serikali ya mseto na maandalizi ya uchaguzi mkuu!!! I doubt it wanachofanya CCM ni delaying tactics kwasababu wanajua wameshawazidi kete CUF katika daftari wanabuy time uchaguzi upite waitishe hiyo serikali ya mseto but CUF wakati huo itakuwa weak waseme hawana nafasi ya kuunda serikali mwisho wa siku inarudi serikali ile ile..

Hizi delaying tactics zinasukwa na CCM bara lakini broo CCM Zanzibar wakiamua jambo huwa hawarudi nyuma ni kama walivyoamua kuchukua mapanga na kufanya mapinduzi, CCM bara wangefanikiwa sana kama wangeshawishi ile hoja isisomwe kwenye BLW lakini sasa is too late
 
You all got it wrong, Zanzibar na BLW wanataka serekali ya umoja wa kitaifa na sio serekali ya mseto....😕
 
You all got it wrong, Zanzibar na BLW wanataka serekali ya umoja wa kitaifa na sio serekali ya mseto....😕

Kaka waswahili wanasema mshika mawili moja humtoka. ZEC ifanye kipi iandae uchaguzi wa taifa???, Ipokee kura za maoni ya serikali ya mseto???, au iendelee na zoezi la daftari la kudumu???

Ndio maana nasema hili ni changa la macho!!!
 
You all got it wrong, Zanzibar na BLW wanataka serekali ya umoja wa kitaifa na sio serekali ya mseto....😕

Which is which MrFroasty and which is not which, what is the difference between serikali ya umoja wa kitaifa na serikali ya mseto pls.
 
Hiki kichwa cha habari ni cha kifitina na cha kupotosha. Ni wapi pameandikwa kuwa Zanzibar inapingana na ZEC-CCM?

Kubwajinga usilete ubishi usio na maana kwa kutumia maneno ya kiukeleketwa (fitina uchochezi na upotoshaji) ina maana hata Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar analeta uchochezi kwa sababu na yeye amepinga maamuzi ya NEC mtajiju CCM bara pamoja na roho zenu za kwa nini wenzenu Zanzibar hawawataki na wanapeta hebu msikilize Spika anavyosema

Kificho(4).jpg


Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, amesema kura ya maoni itakayoamua kuundwa kwa Serikali ya Mseto Zanzibar itafanyika kabla ya uchaguzi Mkuu kama ilivyoamuliwa na Wajumbe wa Baraza hilo Januari, mwaka huu.

Akizungumza na Nipashe jana Zanzibar, Spika Kificho, alisema hakuna mtu mwenye ubavu wa kubadilisha maamuzi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi zaidi ya wenyewe waliopitisha uamuzi huo.

Aliyasema hayo baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichomalizika Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, kiliamua kura ya maoni kuhusu Serikali ya Mseto ifanyike baada ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Alisema kura hiyo ya maoni ndio itakayotoa uamuzi wa kuundwa serikali shirikishi baada ya uchaguzi mkuu iwapo wananchi watakuwa wamefikia muafaka wa kuundwa Serikali ya Mseto.

Alisema hivi karibuni atatangaza majina ya wajumbe sita watakaounda kamati ya kufuatilia utekelezaji wa hoja binafsi ya kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Alisema kamati hiyo itakuwa na wajumbe watatu kutoka CCM na watatu kutoka CUF na ndio watakaopewa jukumu kwa niaba ya Baraza ya kufuatilia hatua za utekelezaji kabla ya wananchi kufikia hatua ya kushiriki katika kura ya maoni.

Spika Kificho alisema jambo linalosubiriwa hadi sasa ni kuwasilishwa kwa muswada wa marekebisho ya sheria utakaoipa mamlaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kusimamia suala la kura ya maoni kabla ya kufikia kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani.

Hata hivyo, alisema bado ni mapema kueleza kwamba muswada huo utawasilishwa katika kikao cha Machi 24 au baadaye kwa vile bado unaendelea kutayarishwa na Mwanasheria Mkuu.

Suala la kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa limefikiwa baada ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitisha hoja binafsi iliyowasilishwa na Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakar.
Hata hivyo, Wajumbe wa Baraza hilo wameitaka Serikali kabla ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuitishwe kura ya maoni, kwa vile suala hilo linahusu katiba ya Zanzibar kama ilivyoamuliwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Butiama mwaka 2008.

Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar unatarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu na iwapo suala hilo litakubalika kupitia kura ya maoni itakuwa ni mara ya kwanza kwa Zanzibar kuundwa kwa Serikali ya Mseto tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi Visiwani mwaka 1992.

CHANZO: NIPASHE
 
Which is which MrFroasty and which is not which, what is the difference between serikali ya umoja wa kitaifa na serikali ya mseto pls.
Kipande cha Makala ya Jabir:

Serikali ya Umoja

Wapo watu hawajaelewa tofauti ya serikali ya umoja wa kitaifa na serikali ya mseto. Hivi ni vitu tofauti kinadharia na kihalisia.

Kwa mujibu wa azimio la Baraza la Wawakilishi, serikali inayohitajika kuwepo Zanzibar ni serikali ya umoja wa kitaifa, siyo ya mseto.

Nilifafanua jambo hili katika kipindi cha Tuongee asubuhi kinachorushwa kila siku na kituo cha televisheni cha StarTV Dar es Salaam, Jumapili.

Serikali ya mseto ni ile inayoundwa na vyama zaidi ya kimoja kikiwemo chama kiongozi katika matokeo ya uchaguzi mkuu lakini hakikupata kura za kutosha kikatiba kukiwezesha peke yake kuunda serikali.

Kwa mfano, tuseme Katiba inasema chama kitakachounda serikali ni kile kilichopata asilimia 50 ya kura zote za bunge. Chama A kimepata asilimia 40 na ndiyo cha juu ya vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi.

Kipo Chama B kimepata asilimia 20 ya kura. Hiki ndio chama cha pili baada ya chama A na kitabaki kuwa chama kikuu cha upinzani bungeni. Chama A kitahitaji asilimia 10 ili kiunde serikali.

Hapa kitalazimika kuomba kushirikiana na chama kimoja au viwili vilivyopata kura chache ya kile chama B ili kufikisha asilimia 50 ya kura zinazotakiwa na katiba kukiwezesha kuunda serikali.

Hii ndio serikali ya mseto. Kwa sasa serikali kama hii ipo nchi nyingi zikiwemo India, Ujerumani na Israel.

Serikali ya umoja wa kitaifa ni ile inayoundwa na vyama zaidi ya kimoja – vyaweza kuwa viwili tu – vilivyoingia katika majadiliano kwa nia ya kutatua mgogoro wa kiuongozi unaokabili nchi. Mfano mzuri ni Kenya na Zimbabwe.

Aghalabu serikali ya aina hii hutokana na muafaka baada ya kutokea mgogoro unaoweza kuwa umesababishwa na mabishano ya matokeo ya uchaguzi au mgogoro wa muda mrefu wa kisiasa.

Zanzibar iliwahi kuwa na serikali ya mfumo huu baada ya uchaguzi wa mwaka 1963. Ilishirikisha vyama vya Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP).

Mohamed Shamte ndiye aliyekuwa waziri mkuu wa serikali hiyo na alifanikisha kuipeleka Zanzibar kwenye Umoja wa Mataifa ambako ilipata kiti chake kama mmoja wa wanachama wa umoja huo.

Serikali hiyo iliyoundwa kufuatia uhuru wa 10 Desemba 1963, iliangushwa baada ya siku 33 tu – kwa mapinduzi ya 12 Januari 1964 – kwa kile kilichoelezwa na waasisi wa Afro Shirazi Party (ASP) kwamba haikuwa serikali halali ya wazalendo bali vibaraka wa utawala wa Kisultani uliokuwa unahifadhiwa na Uingereza.
 
Natamani siku moja spika wetu six angekuwa na courage ya kusema kama hivi

"No person or authority has the power or mandate to overrule a decision passed by the House of Representatives,
Zanzibar House of Representatives Speaker Pandu Ameir Kificho
 
Sasa wadanganyika vipi tena leo hamutetei katiba iheshimiwe tena?

Maana kificho na BLW hawavunji katiba, wanachokifanya ni right kabisa.Baraza hiyo inawakilisha wazanzibari, na uvunjaji wa katiba kujaribu kuingilia maamuzi ya chombo kama hicho.

Same case kwa bunge la TZ, kuanza kumtia mshike mshike Sitta ni ukiukwaji wa maadili na katiba.

Sasa huyo Kificho na Baraza yake wako right, sio Chiligati/Msekwa/Makamba na NEC yao wawe juu ya vyombo vya sheria.

Time will tell, hivyo alivyosema Kificho ndivyo hivyo itakavyofanyika.... 😎
 
Sasa wadanganyika vipi tena leo hamutetei katiba iheshimiwe tena?

Maana kificho na BLW hawavunji katiba, wanachokifanya ni right kabisa.Baraza hiyo inawakilisha wazanzibari, na uvunjaji wa katiba kujaribu kuingilia maamuzi ya chombo kama hicho.

Same case kwa bunge la TZ, kuanza kumtia mshike mshike Sitta ni ukiukwaji wa maadili na katiba.

Sasa huyo Kificho na Baraza yake wako right, sio Chiligati/Msekwa/Makamba na NEC yao wawe juu ya vyombo vya sheria.

Time will tell, hivyo alivyosema Kificho ndivyo hivyo itakavyofanyika.... 😎

MrFroasty sisi huku ni blaa blaa nyingi tu nchi inaongozwa na kaliba za kina Makamba unategemea nini kama si uhasama tu unapokuta viongozi wakuu wanakiri hadharani kuwa wanauhasama jua hakuna maendeleo yoyote I hate the way Msekwa is doing atalipeleka taifa kubaya
 
MrFroasty sisi huku ni blaa blaa nyingi tu nchi inaongozwa na kaliba za kina Makamba unategemea nini kama si uhasama tu unapokuta viongozi wakuu wanakiri hadharani kuwa wanauhasama jua hakuna maendeleo yoyote I hate the way Msekwa is doing atalipeleka taifa kubaya
Its sad unapokuta watu wanashangilia vitendo vinavyofanywa na vikongwe hivyo Msekwa/Makamba kwa kupitia NEC.

Last time I was really pissed kuona Sitta anatishiwa hata kuvuliwa uanachama, ati kwasababu ameacha wabunge kupiga kelele za ufisadi!

Sasa sijuwi hivyo vibabu vilitaka Sitta afanye nini?Wabunge au wawakilishi wanachopigia kelele sio wao personally, HIZO NDIO KELELE ZETU WANYONGE HUKU MITAANI!!

Sasa hiyo kesi ya BLW, sisi wazanzibari wote tunataka GNU ianze hata kesho...wao { NEC/Msekwa/Makamba/Chiligati } wanataka uchaguzi kwanza halafu ndio tusubiri refferendum.

Sasa tukishaingia kwenye uchaguzi na mchakato ulioko kwenye daftari lililoliwa na buku, si hii nafasi ya kuleta maelewano visiwani ndio ishatutoka?

Mie nataka wadanganyika mufahamu hizo mshike mshike za uchaguzi sio Seif anaepata kipigo, hapo hizo harakati za siasa wanaopoteza na kuchapwa ni raia wa mitaani....hebu rudieni hizo video za miaka iliopita, utakuta jamaa mmoja amevaa t-shirt nyekundu...huyo jamaa ana matatizo ya akili/mwendawazimu anakula kichapo heavy kutoka kwa FFU.

Last time kulikuwa na video mama fulani anakula kichapo, nae pia ni mgonjwa wa akili...sasa athari za vugu-vugu la kisiasa halimuathiri mtu bali ni wananchi wa chini wasio na hatia....ofcourse Seif ni waziri mstaafu analindwa, jee hawa wananchi nao wanalindwa na nani???

Waacheni huko barazani wafanye maamuzi, sio kembele-mbele kama mifuko ya shati 😎
 
Makamba Msekwa na NEC yao wanatamani referendum ifanyike baada ya uchaguzi ili wafanye mambo yao ionekane CCM zanzibar imeshinda kwa kura nyingi hivyo hakuna haja ya Mseto lakini issue ikastukiwa na wazenji wakaiwahisha BLW mchezo ukaishia hapo sasa kama wana ubavu waingie humo barazani wakawagawe kama wanaweza but i think it is too late my dear poor Msekwa
 
mbona mnachanganya madawa nyie .serikali ya kitaifa na mseto is the some thing,kawaida ninavyojua mimi mseto ni mix ya mchele na choko .it all depend what you wanna call it.
 
mbona mnachanganya madawa nyie .serikali ya kitaifa na mseto is the some thing,kawaida ninavyojua mimi mseto ni mix ya mchele na choko .it all depend what you wanna call it.
Naona wewe ndiye unayeyachanganya. Mseto ni mseto kwa lugha ya kawaida. Lakini mseto katika hali ya Zenj kweli unachanganya.
CUF wanatamani mseto wa aina fulani.
CCM(Bara) wanatamani mseto wa aina fulani pia.
CCM (Zanzibar ) nao pia wanatamani mseto wa aina fulani
Lakini Baraza la Wawakilishi ( Na fikiri pia SMZ) wameamua mseto wa aina fulani. Tofauti na matamanio ya wote hao hapo juu. sasa ngoma uwanjani
Nseto huo !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!![/B
 
sasa mseto huo utakuwa vipi ikiwa kila chama kina sera zake and different believes .kwa mfano CUF wanaamini kwamba uhuru ulipatikana 10/12/1963 na CCM wao wanasema uhuru ulipatikana january 12 1964.
 
sasa mseto huo utakuwa vipi ikiwa kila chama kina sera zake and different believes .kwa mfano CUF wanaamini kwamba uhuru ulipatikana 10/12/1963 na CCM wao wanasema uhuru ulipatikana january 12 1964.

A country get independence only once and that is 1963.

1964 was a revolution to overthrow Zanzibar government which was granted independence by the British on 1963.

Thats what make sense...you really have to come with critical explanation/theory to convince the world otherwise...and if you do, you probably have your own agenda 🙄
 
Back
Top Bottom