Zanzibari kukataza wanaume kusuka sio jambo la kimaadili ila ni chanzo kipya cha uchumi

Zanzibari kukataza wanaume kusuka sio jambo la kimaadili ila ni chanzo kipya cha uchumi

Maco marco

Senior Member
Joined
Jun 10, 2023
Posts
108
Reaction score
86
Labda ningependa kuwatafakarisha watanzania wenzangu kwa jambo hili.

Hivi tunaweza kutoza shilingi ngapi ili kuruhusu mtu kuzidisha mwendo kasi kwenye barabara za makazi ya watu? Au kumruhusu mtu kukata viungo vya albino? Au kufanya uwindaji haramu kwenye mbuga na bahari?

Ninacho jaribu kusema hapa hukuna thamani katika kuvunja sheria...Hata zile issues za faini ni adhabau baada ya kuvunja sheria ili kuonesha kwamba mshitakiwa anatakiwa ajutie kwa kosa alilofanya.

Sasa ndugu zetu wazanzibari wanasema kwamba kwa maadili yao ni kosa kwa mwanaume kusuka, lakini kama atanunua kibali kwa kulipia kwa kulipia tsh.1 m anaweza kusuka.

Na tunafahamu kwamba maadilia hayo yanahusishwa moja kwa moja na imani ya dini ya kiisilamu ilyotawala visiwani humo. Sasa je wanataka kusema nini, kwamba sheria za mungu zinaweza zikawa na thamani(kununulika) kwa anaetaka kuzivunja, hivi ndivyo inavyo eleweka.

Kwa kifupi sheria hii imemdhalilisha mungu na kuonesha kuwa kumbe maadili ya mungu yanaweza kuvunjwa kama tu ukiwa na fedha.

Kilichofanyika sasa sio kulinda maadili bali nikuliongezea thamani swala wanaume kusuka.. Mwanaume wakizanzibari akisuka leo ataonekana ni mtu mwenye hela hivyo itainua hadhi yake katika jamii nakumfanya kuwa role model wa watoto wengi zaidi wanaotamani wakipata pesa wawe kama yeye, je lengo la kukuza maadili liko wapi hapa.

Kama wanataka kulinda maadili kweli wanatakiwa wapinge kabisa swala la wanaume kusuka na waweke sheria kali kwa kila atake vunja, hapo wataweza kusema wana linda maadili lakini kwa kuweka mwanya kwa watu kuendelea na tabia ileile tena kwa fedha sio kulinda maadili bali waseme tu wameongeza vyanzo vya mapato na wapewe sifa kisiasa na si katika majukwaa ya mambo ya kimaadili.

Pia Soma:
- Baraza la Sanaa-Zanzibar: Wanaume Wanaosukwa kama Wanawake kukamatwa, kibali cha kusuka ni Tsh. Milioni 1

Kwa marufuku nyingine Zanzibar soma:

Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika

 
Back
Top Bottom