Zao la kumnyima Haji Manara nakala ya hukumu hili

Zao la kumnyima Haji Manara nakala ya hukumu hili

Cheupe alishasema ukiishabikia Utoo tuu unakua na akili za kipoyoyoo
Na bado anazidi kupata wafuasi mapoyoyo wenziee
 
Vipi Nako kushabikia mikia fc🦁./Lunyasi🚶
Kushabikia simba ni jambo jema ni kama vile mtu aliyefanikiwa kupata mwenza wa kufanana naye.

Tatizo la Yanga ni kutoheshimu taratibu na miongozo hata wanayojiwekea.

Haji Manara na Hassan Bumbuli nani msemaji rasmi wa klabu?
 
Ndugu usitaje uzeruzeru maana hakupenda azaliwe hivyo ni kazi ya Mungu, kumbuka wewe unazaa pia, utakuja zaa zeruzeru
Ila yeye kukejeli maumbile ya wengine wewe unaona poa? Unakumbuka alikuwa anamuita Mwakalebela kilo 800? Hivi Haji Manara ndiye zeruzeru pekee katika nchi hii, mbona wengine hawakejeliwi? Ukiishi kwenye nyumba ya kioo usianze kuwarushia watu nawe.
 
Na mie Nakazia 'Huyu ni Zeru Zeru Mkaidi tu'....! Mkuki Kwa kitimoto mtamu..Kwa Binadamu Uchungu EE..!
 
Maneno mnayo nyie wapambe wake ,huko alikoyakanyaga anaenda kupokea nyundo tu.
Sijawahi kuwa mpambe wa kiumbe chochote kile hapa duniani. Mimi ni mtu nisiyeweza kuvumilia uonevu.

Sijawahi kuzikubali kejeli na maneno ya kuudhi ya Haji Manara, lakini ni lazima ukweli usemwe! Adhabu aliyopewa ilijaa mihemko, ya kumkomoa, na ilitaka kutuaminisha kwamba Wallace Karia ni mtu mkubwa sana, hata kama na yeye anafanya makosa, hawezi kuadhibiwa! Kitu ambacho si sahihi hata kidogo.

Maana angekuwa ni mtu mwenye mamlaka makubwa kiasi hicho, asingepata muda wa kutupiana maneno na mtu kama Haji Manara kwenye mechi ambayo huyo Wallace Karia alikuwa akishangilia Coastal Union, huku Haji Manara akishangilia Yanga.
 
Ndiko tunakoelekea wee Ngoja muda utaongea tu. Tff wabachokitafuta kipo karibu.
 
Chanzo chote Ni viongozi kutotambua nafasi zao, Karia ushabiki wako kwa timu flani utakumaliza. Tambua nafasi uliyokuwa nayo, mapenzi yako na ushabiki wako weka pembeni otherwise anguko lako li karibu Sana.
 
Mnavyojua kujidanganya sijui mlisomea wapi!
Anaye jidanganya ni nani sasa! Si muwashawishi hao mashabiki wenzenu wampe adhabu! Mimi nimetoa tu mtazamo wangu.

Hiyo jeuri ya kumuadhibu hawana. Kwa sababu hata hiyo adhabu yenyewe aliyopewa huyo Haji Manara, ilijaa mihemko.

Kosa alilofanya CEO wenu Barbara kwa yule Afisa wa TFF na hili la Manara, lipi lilikuwa ni kubwa zaidi? Vipi adhabu zao zinalingana? Wadau wengi wa michezo tunaka kuona TFF inatumia muda wake mwingi kwenye kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kanuni za mpira wa miguu! Na siyo kujikita kwenye siasa za kipuuzi za usimba na uyanga.
 
Back
Top Bottom